Na Veronica Simba – Ukerewe
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani amewataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini nchini kote, kuwasilisha mipango-kazi yao kwa viongozi na wawakilishi wa wananchi wa maeneo wanakofanyia kazi ili waweze kuielewa hivyo kusimamia utekelezaji wake.
Alitoa maagizo hayo jana, Desemba 30, 2018 wilayani Ukerewe akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme pamoja na kuzungumza na wananchi.

Akizungumza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ofisini kwa Mkuu wa Wilaya, Colonel Magembe, Waziri Kalemani alifafanua kwamba viongozi na wawakilishi wa wananchi ndiyo wanawajibika kuisemea serikali, hivyo wanapaswa kuifahamu kwa kina miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao, waweze kuwaeleza wananchi.

“Hili ni agizo kwa wakandarasi wote wa miradi hii nchi nzima, wapatieni viongozi wa maeneo mnayofanya kazi mipango-kazi yenu, wajue nini mnatekeleza, kwa namna gani na kwa kipindi gani ili nao wasaidie kuwaelimisha wananchi wao,” alisisitiza Waziri.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chabilungo wilayani Ukerewe, Desemba 30, 2018 kabla ya kuwasha rasmi umeme katika eneo hilo, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.
 Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani (wa pili-kulia) akikata utepe kabla ya kuwasha rasmi umeme katika Shule ya Msingi Chabilungo wilayani Ukerewe, Desemba 30, 2018, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme. Kulia ni Mkuu wa Wilaya, Colonel Magembe na kushoto ni Mwalimu anayefundisha shuleni hapo.
Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani, akimweleza dhamira ya ziara yake, Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Colonel Magembe (kushoto) pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alipowasili wilayani humo Desemba 30, mwaka huu, kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...