Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), akielezea kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019 katika kipindi cha Julai-Novemba, 2018), ambapo alisema Tanzania inaendelea kuwa miongoni mwa nchi tano zinazokua kwa kasi kiuchumi Barani Afrika, wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.
Baadhi ya Viongozi wa Wizara ya Fedha na Mipango na Wadau wengine wakifuatilia kwa makini Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa na utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2018/2019, kwa kipindi cha Julai - Novemba, 2018, wakati wa Mkutano kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waandishi wa Habar,i katika Ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma. 
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (katikati), akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari Jijini Dodoma, kuhusu ufadhili wa wahisani ambapo alisema Wahisani wengi wanamasharti magumu hivyo akasisitiza umuhimu wa wananchi kulipa kodi ili nchi iweze kujitegemea. 
Meza Kuu ikiongozwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango(Mb), (katikati), wakifuatilia kwa makini baadhi ya maswali ya Waandishi wa Habari kuhusu taarifa iliyotolewa ya Hali ya Uchumi wa nchi na Utekelezaji wa Bajeti Kuu ya Serikali, katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dodoma.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...