Na Abullatif Yunus wa Michuzi Blog,  Kagera. 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola, ameanza Rasmi ziara yake Mkoani Kagera kwa kukutana na Idara pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo, na kisha kufanya Mkutano wa hadhara licha ya Mkutano huo kuchelewa kutokana na Majukumu yaliyokuwepo.

Mh. Kangi Lugola katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi wa Utekelezaji unaofanywa na Mh. Rais John Pombe Magufuli, katika Kusimamia Amani ya Nchi na Watanzania kwa Ujumla, na kuwa Mh. Rais hapendi kusikia Mwananchi yeyote akionewa, na kunyimwa haki kwa namna yoyote ile.

Sambamba na hilo Mh. Waziri Lugola, katika kuwakumbusha Watendaji na watumishi ndani ya Vyombo vya Ulinzi vya Usalama kuendelea kutenda haki na kulinda Amani bila kuchoka, isipokuwa wale wachache ambao wamekuwa wakichafua Vyombo vya Ulinzi kutafuta Kazi nyingine ya kufanya, akitolea mfano baadhi ya Askari wa Jeshi la Polisi wanaofukuza Bodaboda, na kukamata Bodaboda Gulioni.

Kuhusu Wananchi wanaowakaribisha Raia wasio Watanzania na Wahamiaji haramu amewatahadhalisha wenye kufanya hivyo waache Mara moja kwani kwa kufanya hivyo ni kuhatarisha Usalama wa Nchi yetu, ikiwa ni sambamba na wale wanaofanya shughuli za magendo.

Katika Mkutano huo wa hadhara Mh. Waziri Lugola amepata nafasi ya kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa Wananchi nakuahidi kuzishughulikia ndani ya muda mfupi kabla hajaondoka Mkoani Kagera.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Kangi Lugola akizungumza na Wananchi waliohudhuria kumsikiliza katika Uwanja wa Mayunga Mjini Bukoba. 
 Bi Sauda Amiri (34) Mkazi wa Bukoba Manispaa, Akitoa kero yake kwa Mh. Lugola juu ya Uonevu aliofanyiwa kwa kuchomewa Nyumba yake pamoja na kufyekewa shamba lake la miche ya nyanya 1500.
 Sehemu ya Umati uliojitokeza katika Viwanja vya Mayunga Bukoba kumsikiliza Mh. Kangi Lugola Januari 2, 2019.
Picha na Abullatif Yunus wa Michuzi Blog,  Kagera.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...