Na Abdulatif Yunus wa Michuzi Blog, Kagera
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Mkoani Kagera, imehitimishwa Januari 02, 2019 kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa Mkoani Kagera, imehitimishwa Januari 02, 2019 kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Katika Mkutano huo pamoja na mambo mengine, Dkt. Bashiru amehitimisha kwa kuwataka wajumbe wa Kikao hicho kusitisha mchakato na mgogoro uliokuwa ukifukuta ndani ya CCM, baina ya Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mh. Jasson Rweikiza pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba, Ndg. Murshidi Ngeze kuacha Mara moja kwani hauna tija wala faida ndani ya Chama, zaidi ni kuzorotesha Maendeleo.
Akirejea mgogoro huo kabla ya kusuluhisha, amenukuliwa akisema kuwa kumekuwepo na hali isiyokuwa ya kawaida kati ya Madiwani wanoumuunga mkono Mbunge na wale wanaomuunga mkono Mwenyekiti kuhusu wapi ijengwe Hospitali ya Wilaya ya Bukoba.
Katibu Bashiru amethibitishia Kikao juu ya Kuomba radhi na Kukiri mbele ya Kamati ya Siasa kwa Mwenyekiti kuwa aliyumba kimaamuzi licha ya suluhisho kupatikana kuwa Hospitali ijengwe eneo la Kanazi kulingana na hoja za kitaalamu na Ukubwa wa eneo husika.
Kufuatia maelezo hayo Viongozi hao wawili Mbunge na Mwenyekiti wakapata nafasi ya kujieleza na kisha kumaliza tofauti zao za kisiasa huku Katibu Mkuu akimuomba Ndg. Rweikiza (MB) kurudisha malalamiko yake ndani ya Chama na sio Mhakamani kwa kile anacholalamika kuwa Ndg. Ngeze (Diwani Kata Rukoma) alimdhalilisha kwa kumtuhumu kuwa Mbunge Rweikiza alitoa Rushwa katika mchakato wa Uchaguzi.
Tayari Mh. Rweikiza amekubali kurejea kwenye Vikao vya suluhisho na maadili ya Chama kulalamika upya, ingawa Dkt. Bashiru kaelekeza Viongozi hao kwenda kutoa ufafanuzi mzuri eneo la Ikimba ambalo baadhi ya watu walipotosha kuwa wametengwa kufuatia Hospitali kutojengwa eneo lao.
Aidha Dkt. Bashiru amepata nafasi ya kuwakaribisha rasmi madiwani waliorudi kutoka Vyama pinzani, huku kivutio kikubwa akiwa ni Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Kapteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi Ndg. Kateme ambae baada ya kushindwa katika kinyanganyiro cha Uchaguzi katika Kara ya Kaibanja, alitimkia CUF na sasa ameamua kurejea kutokana na kuridhishwa na muundo wa Serikali iliyopo madarakani, na Utendaji kazi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa akizungumza wakati akihitimisha ziara yale leo Bukoba mkoani Kagera kwa kukutana na Viongozi, Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini, katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Baadhi ya Wanachama na wajumbe wa Halmashauri ya Wilaya Bukoba Vijijini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Taifa, Dkt. Bashiru Ally Kakurwa katika Kikao chao kilichofanyika katika Ukumbi wa Bukoba Coop Mjini Bukoba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...