Na Veronica Simba – Geita
Wizara ya Nishati inatekeleza mkakati wa kuwaunganishia umeme wa uhakika wachimbaji wadogo wa madini kote nchini, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais John Magufulu kuiwezesha sekta hiyo izalishe kwa tija kwa manufaa yao binafsi na ya Taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu, kinachomilikiwa na kampuni ya Padalu, kijijini Lumasa, Chato; Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa eneo hilo, Dkt Medard Kalemani, alisema serikali imefunga transfoma tano zenye uwezo wa KVA 400 hadi 1,000 ili kuwawezesha wachimbaji wadogo wa Geita kuzalisha kwa tija.
“Umeme huu mkubwa utawawezesha wachimbaji kuchimba , kuchenjua na kuongeza thamani dhahabu yao ili kuiongezea thamani, iwapatie faida na waweze kulipa kodi na mrabaha serikalini,” alisema.
Akieleza zaidi, Waziri Kalemani alisema yako maeneo mkoani humo ambayo bado hayajafikiwa na huduma hiyo lakini akabainisha kuwa utaratibu wa kufunga transfoma nyingine tano zenye uwezo uleule, unafanyika ili kuyafikia maeneo ya wachimbaji yaliyosalia ikiwemo Mbogwe na Nyakafuru.
Waziri
wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (kushoto)
na Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko (kulia), wakifungua kitambaa
maalum kilichofunika jiwe la msingi la kiwanda cha uchenjuaji dhahabu
cha Padalu, kilichopo Chato Geita, kuashiria uzinduzi rasmi. Hafla hiyo
ilifanyika Januari 2, 2019.
Msimamizi
wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita,
Abel Lucas (kulia), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri wa
Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani pamoja na
Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, na ujumbe waliofuatana nao, wakati
wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2, 2019.
Msimamizi
wa Kiwanda cha kuchakata dhahabu cha Padalu, kilichopo Chato Geita,
Abel Lucas (kushoto), akitoa maelezo jinsi kinavyofanya kazi kwa Waziri
wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (wa kwanza
kulia) pamoja na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko (wa pili – kulia),
wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi wa kiwanda hicho, Januari 2,
2019.
Waziri
wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani
(katikati), akisalimiana na Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko
(kushoto), walipowasili kwenye hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika
kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo Chato Geita, Januari
2, 2019. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhandisi Msafiri Mtemi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri
wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani
akizungumza na wananchi, wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi
katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Padalu kilichopo jimboni mwake,
Chato Geita, Januari 2, 2019.
Sehemu
ya umati wa wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati ambaye pia ni
Mbunge wa Chato, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati wa hafla
ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha
Padalu kilichopo jimboni humo, Chato Geita, Januari 2, 2019.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...