WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amefungua mradi wa maghala ya kuhifadhi nafaka na
soko la mazao la OTC-Lilambo katika Halmashauri ya Songea uliogharimu
sh. bilioni 1.5.
Amesema Rais Dkt. John Magufuli ameazimia kuwawezesha wakulima kuwa na mahala pa uhakika pa kuhifadhia mazao yao na sehemu ya kufanyia biashara ili kuwaongezea tija.Amefungua soko hilo leo (Alhamisi, Januari 3, 2019) akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi ya siku nne ya kukagua shughuli za maendeleo mkoani Ruvuma.
Waziri Mkuu amesema ameridhishwa na ujenzi wa soko hilo pamoja na maghala kwani umezingatia viwango. Maghala hayo mawili yana uwezo wa kuhifadhi tani 5,000 za nafaka.“Licha ya soko hili kuwapa wakulima wetu fursa ya kupata masoko ya kuuzia mazao yao, pia watapata mafunzo ya namna ya kuhifadhi bidhaa zao pamoja na taarifa za masoko.”Kadhalika, Waziri Mkuu ameiagiza bodi ya soko hilo kuhakikisha inatoa matangazo katika vyombo mbalimbali vya habari ili wakulima waweze kupeleka mazao yao sokoni hapo.

Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Soko la Mazao la
OTC Lilambo wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Watatu kushoto ni
Waziri wa kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,
Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa Viti Maalum, Jacqueline Ngonyani
Msongozi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Soko la Mazao la
OTC Lilambo wilayani Songea Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu, ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Kulia ni
Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika ya mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro, wapili
kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme na kulia ni Mbunge wa
Viti Maalum.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilitokana na unga
wa mhogo vilivyoandaliwa na kikundi cha wanamawake wajasiriamali
cha Muungano - Mpandagindo, wakati lipofungua Soko la Mazao la OTC
Lilambo wilayani Songea, Januari 3, 2019. Kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,
Christina Mndeme. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Ghala
lenye uwezo wa kuhifadhi tani 5000 za nafaka la OTC Lilambo wilayani
Songea ambalo lilifunguliwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Januari 3,
2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama vyakula mbalimbali vilivyoandaliwa na
kufungashwa kitaalam na Mtandao wa Wajsiriamali Wadogowadogo Ruvuma
(MWARU) wakati alipofungua Soko la Mazao la OTC Lilambo
wilayani Songea, Januari 3, 2019. Wapili kushoto ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu,
Jenista Mhagama na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme.
Kushoto ni Mkurugenzi wa Mtandao wa MWARU, Lucida Chowo (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu) .
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...