Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji Kibaha na
Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wakati wa kikao kazi cha Naibu Waziri
huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa
watumishi hao, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri hizo mkoani Pwani.
Baadhi ya watumishi wa umma wa
Halmashauri ya Mji Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha
wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) (hayupo pichani),
wakati wa kikao kazi cha watumishi hao na Naibu Waziri huyo chenye
lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi hao, kabla ya kukagua
utekelezaji wa miradi ya TASAF katika Halmashauri hizo mkoani Pwani.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Bi.
Theresia Mbando akitoa neno la utangulizi kumkaribisha Naibu Waziri,
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe.
Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) kuzungumza na watumishi wa Halmashauri ya Mji
Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha, wakati wa kikao kazi cha
Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi hao, kabla kukagua utekelezaji wa miradi ya TASAF katika
Halmashauri hizo mkoani Pwani.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) akitoa onyo kwa Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kibaha, Bi. Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na
Rasilimaliwatu wa Halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu mstaafu
aliyekuwa akidai haki yake, onyo hilo amelitoa wakati wa kikao kazi cha
Naibu Waziri huyo na watumishi hao chenye lengo la kuhimiza uwajibikaji
kwa watumishi hao.
……………………
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary
Mwanjelwa (Mb) amempa onyo kali Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kibaha, Bi. Ruth Mwelo ambaye ni Mkuu wa Idara ya Utawala na
Rasilimaliwatu wa Halmashauri hiyo kwa kumtolea lugha chafu mstaafu
aliyekuwa akidai haki yake na kumtaka afisa huyo ajirekebishe haraka
iwezekanavyo.
Onyo hilo amelitoa wilayani
Kibaha, wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Mji wa
Kibaha na Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha chenye lengo la kuhimiza
uwajibikaji, kabla ya kutembelea wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya
Maskini katika wilaya hizo ili kujiridhisha na utekelezaji wake.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema,
haiwezekani afisa huyo mwenye dhamana ya kusimamia Sheria, Kanuni na
Taratibu za kiutumishi ndio awe kikwazo cha utendaji kazi katika
Halmashauri hiyo kwa kutoa lugha chafu dhidi ya wanaofuta huduma ofisini
kwake, na kuongeza kuwa, afisa huyo ndiye anayestahili kuwa kwenye
Kamati ya Maadili ili kutoa miongozo ya uadilifu na kusimamia maadili ya
watumishi kwa ujumla katika Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha.
Mhe. Dkt. Mwanjelwa amemtaka afisa
huyo kutotumia cheo chake vibaya na badala yake asimamie vema nidhamu
na masilahi ya watumishi wa umma.
Sanjari na hilo, Mhe. Dkt.
Mwanjelwa amemtaka afisa huyo kuacha tabia ya kutoa siri za ofisi na
kutokuwa mchonganishi miongoni mwa watumishi wenzie kwani matendo hayo
hayapaswi kufanywa na mtumishi yeyote nchini.
Aidha, Mhe. Dkt. Mwanjelwa amesema
ameamua kuweka bayana mapungufu ya afisa huyo mbele ya watumishi
wenzie ili ajifunze kutokana na matendo yake yasiyoridhisha na aweze
kubadili mwenendo wake mbaya wa kimaadili.
Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb)
ameendelea kuhimiza uwajibikaji kwa watumishi wa umma nchini, kwa kutoa
onyo kwa watumishi wote wanaobainika kukiuka Kanuni za Maadili ya
Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...