Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua kwa kuwa mstari wa mbele katika suala zima la kuwainua Wanawake, Vijana na Walemavu ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa katika makundi hayo ndani ya kipindi cha 2017 – 2018.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo leo wakati akihutubia wananchi kwenye uwanja wa Kolimba, Kaliua moani Tabora.
Aidha katika hatua nyingine Makamu wa Rais ameridhia kuondolewa mara moja kwa Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Kaliua Mhandisi Fikiri Samadi baada ya kushindwa kutekeleza mradi wa maji wa shilingi bilioni 1.5.
“Ziara hizi ni ziara za kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na serikali imekuwa mstari wa mbele kuweka pesa nyingi kwenye miradi ya maendeleo hivyo yeyote atakayekwamisha atachukuliwa hatua mara moja”alisema Makamu wa Rais.
Makamu wa Rais amesema wilaya ya Kaliua ni mfano wa kuigwa kwa kujenga jingo la upasuaji pamoja na wodi ya wazazi yenye uwezo wa kuchukua vitanda 24 katika kituo cha afya Kaliua kwa mapato yao ya ndani pamoja na michango kutoka chama cha msingi Nsungwa ambapo mpaka kukamilika wametumia shilingi 159,703,199.98.
Kwa upande mwingine Naibu Waziri TAMISEMI amesema vikundi vinavyopewa mikopo na Halmashauri lazima virejeshe mikopo hiyo ili iweze kuwasaidia watu wengine akizungumzia kwa wilaya ya Kaliua peke yake ambapo zaidi ya milioni 450 zimetolewa mpaka sasa zimerudishwa milioni 89 tu.
Akizungumzia suala la uchaguzi katika kata 3 za Igombe Mkuluu, Mirambo na Kanindo zilizopo katika jimbo la Ulyankulu, Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Waitara amesema lazima usalama wa Taifa uzingatiwe na upewe kipaumbeke kwani kwenye maeneo hayo kuna waliopewa uraia na kuna wakimbizi hivyo Serikali itakapojiridhisha wanaweza shiriki katika uchaguzi ujao.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya namna ya kutengeneza sabuni bora kutoka kwa
Mwenyekiti wa kikundi cha Wazalendo Ndugu Imani Matabula wakati wa
maonyesho yua wajasiriamali katika viwanja vya Kolimba wilaya ya Kaliua
mkoa wa Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Kaliua na Waziri wa Zamani
katika Wizara mbali mbali Profesa Juma Kapuya(kushoto) mara baada ya
kumaliza kuhutubia wananchi katika uwanja wa Kolimba wilaya ya Kaliua
mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara (kushoto) kabla
ya kuhutubia wa mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kolimba wilaya ya
Kaliua mkoani Tabora. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...