Mume wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja wa Uhusiano Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) Akiwa na Watoto wake wakitoa Heshima ya Mwisho kwenye ibada ya kuaga Marehemu huyo katika Kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach Jijini Dar es Salaam, ambapo Marehemu amaeagwa hapo na wakazi wa Dar es Salaam kisha kusafirishwa kwenda kuzikwa nyumbani kwao Mikese Morogoro.
Wahubiri wakitoa Baraka na Heshima za Mwisho kwa Mwili wa Marehemu Glory Mziray ambae alikuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS).
Watoto wa Marehemu Glory Mziray wakiongoza mbele na Msalaba wakati wakiondoka Katika Kanisa la KKT Usharika wa Mbezi Beacha Kuelekea Mjini Morogoro.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora ,Dk Mary Mwanjelwa akitoa Salamu Kabla ya kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray aliyekuwa Meneja Mahusiano wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini (TFS) ,Dk.Mwanjelwa amezungumzia jinsi alivyo mfahamu Mziray tangu alipokuwa nae katika Chuo kikuu cha Mtakatifu agustino na kutaja umhiri wake katika kutimiza wajibu na majukumu anayopewa.
Mkurugenzi wa Huduma za Misitu ,Emmanuel Willfred, akizungumza na kutoa wasifu wa Marehemu Glory Mziray enzi za uhai wake katika eneo lake la kazi kama Meneja wa Mahusiano.
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Tume kudhibiti Ukimwi Tanzania(TACAID'S),Fatuma Mrisho akizungumza juu ya uzoefu wake katika kazi na Marehemu Glory Mziray.
Sehemu ya Wafanyakazi wa TFS wakitoa heshima za Mwisho kwa Marehemu Glory mziray
Sehemu ya Watu mbalimbali waliojitokeza kuaga Mwili wa Marehemu Glory Mziray katika ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Mbezi Beach.
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMIA
ya waombolezaji wamejitokeza kwa wingi katika Kanisa la KKKT lililopo
eneo la Tangi Bovu jijini Dar es Salaam kuaga mwili wa aliyekuwa Meneja
Habari na Mawasiloano wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS)
Groly Mziray
Groly
Mziray ameagwa leo Februari 21 ,2019 kanisani hapo kuanzia saa saba
mchana baada ya kufanyika ibada maalumu.Marehemu Groly atazikwa kesho
Ijumaa huko Mikese mkoani Morogoro. Baada ya mwili wake kuagwa kanisani
hapo safari ya kuelekea Mikese ilianza. Glory alizaliwaDesemba 27, 1980 na ameacha mume na watoto wawili.
Wakati
wa kumuaga vilio,simanzi na majonzi vilitawala Kanisani hapo kutokana
na baadhi ya waombolezaji kushindwa kujizuia maumivu yaliyopo moyoni
kutokana kifo cha ghafla kwa Groly Mziray.
Baadhi
ya waombolezaji wameiambia Michuzi Blog kuwa kifo cha Groly ni pigo
kubwa kwao na eneo ambalo alikuwa anafanyia kazi na watamkumbuka kwa
namna ambavyo aliamini katika kufanya kazi kwa bidii na hakuwa mwenye
kukata tamaa.
Akimzungumza
mbele ya waombolezaji, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara kutoka Wakala
wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Wilfred Emmanuel amesema Groly Mziray
alikuwa ni mtumishi aliyekuwa anajitoa kwa dhati kwa ajili ya taasisi
hiyo na kubwa zaidi alikuwa na mikakati yenye lengo la kuhakikishia
taasisi yao inapiga hatua zaidi katika kutoa huduma.
Amefafanua
wiki iliyopita walikuwa naye Morogoro kwa ajili ya kuandaa bajeti na
anakumbuka kwenye kikao hicho Groly alitoa maoni na mipango yenye
kuifanya TFS inatekeleza majukumu yake vizuri.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala bora, Dk.Mary Mwanjelwa ameeleza Groly enzi za uhai wake
alikuwa mtu mwenye jitihada na kupenda kujifunza na alipenda kusaidia
wengine.
Amesema
kuwa yeye alisoma na Glory Shahada ya pili na walipokuwa darasani
alikuwa ni mwenye kujituma."Alipenda sana kujifunza na kushirikiana na
wenzi.Ni mtu mwenye kusimamia haki na alikuwa na upendo sana".
Wakati
huo huo Msemaji wa Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam,Tabu Shaibu
amesema kuwa Groly ni kati ya watu waliokuwa mfano kwani alikuwa
mpambanaji na hakuwa mwenye kukubali kushindwa na hasa katika mambo
ambayo aliona yana tija.
"Kwangu
Groly mbali ya kuwa mtumishi mwenzetu akihudumu TFS lakini alikuwa
mdogo wangu.Kwa kweli ameondoka tukiwa bado tunamuhitaji lakini
tumshukuru Mungu kwa kutupa Groly ingawa leo hii hatunaye tena hapa
duniani.Nenda mdogo wangu ,tutakukumbuka daima," amesema Shaibu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...