Na Leandra Gabriel, Blogu ya Jamii
MBUNIFU maarufu duniani na Mkurugenzi wa kampuni za Chanel na Fendi Karl Lagerfeld (85) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Vyombo vya habari nchini ufarasa vimeeleza kuwa Karl hajaonekana katika matukio makubwa ya mitindo tangu mwezi uliopita likiwemo lile la Channel na alilazwa katika hospitali ya Paris na kuruhusiwa na umauti kumkuta jana kabla ya kulazwa huku chanzo cha kifo chake hakijathibitishwa.
Wanamitindo wakubwa wakiwemo Kim Kardashian, Victoria Beckham na Donatella Versace wametoa salamu za rambirambi kutokana na kifo cha mbunifu mkongwe ambaye alifahamika zaidi kwa kuvaa miwani nyeusi na mtindo wa ubanaji wa nywele.
Wengi wa watu maarufu wamemuelezea Karl kama mtu mcheshi na mkarimu kuwahi kutokea, na tasnia ya mitindo na ubunifu imepata pengo kubwa sana.
Lebo ya Fendi imekuwa maarufu zaidi duniani kote ikiwemo nchini huku nchini China ikishika kasi tangu mwaka 2007.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...