| WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akizungumza mara baada ya kutembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza wakati wa ziara yake mkoani Tanga |
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kushoto akimsikiliza
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu
| MKUU wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza wakati wa ziara hiyo |
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa akishuka kwenye tanki
kubwa la kuhifadhia maji eneo la Kilapula Jijini Tanga ambayo yatatoka
eneo la Pongwe kuelekea wilayani Muheza kupunguza changamoto ya uhaba
wa maji kwenye wilaya hiyo
Mabomba yakiwa yameweka eneo hilo mradi huo mkubwa ukiendelea
kutekelezwa
Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly kushoto akiwa
na katibu wa Mbunge wa Jimbo la Muheza kulia kushoto ni PRO wa Mamlaka
hiyo Dorrah Killoh
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa kulia akionyeshwa kitu
kwenye ramani na Mhifadhi wa Misitu ya Amani wilayani Muheza Mwanaidi
Kijazi katika wakati alipotembelea chanzo kikubwa cha Maji wilayani
Muheza cha Amani kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mhandisi Mwanasha
Tumbo kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey
Hilly
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame Mbarawa katikati
akisisitiza jambo kwa viongozi wa wilaya ya Muheza mara baada ya
kutembelea chanzo hicho
WAZIRI wa Maji Proffesa Makame
Mbarawa amesema serikali kupitia mamlaka za maji watahakikisha
wanapeleka huduma ya maji safi na salama kwenye vijiji vilivyopo
karibu na vyanzo vya maji ili waendelee kuvitunza viweze kusaidia
vizazi vya sasa na vijavyo.
Mbarawa aliyasema hayo wakati
alipotembelea chanzo cha Maji cha Amani wilayani Muheza mkoani Tanga
ikiwa ni ziara yake ya siku ya pili mkoani hapa ambapo aliwataka
wananchi kulinda vyanzo
Alisema haitakuwa na maana iwapo
wananchi hao wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji lakini hawana maji
safi na salama hivyo watahakikisha nao wanapata huduma hiyo muhimu kwa
ustawi wa maisha yao na jamii zao.
Alieleza kwa sababu
mwaka 1962 maji yaliyo yakipatikana kwa mtu mmoja yalikuwa mita za
ujazo 7862 hivi sasa mtu mmoja kwa mwaka anaweza kutumia maji yaliyopo
mita za ujazo 1800 lakini siku hizo kulikuwa na watu milioni 10.6
lakini leo hii watu zaidi ya milioni 50 na watu wanazidi
kuongezeka.
“Ndugu zangu Serikali kupitia mamlaka za Maji tutahakikisha
wananchi wanaoishi karibu na vyanzo vya maji wanapata huduma ya maji
safi kwa maana haitakuwa na maana kama wataendelea kuvitunza vyanzo
hivyo wakati wao hawapati maji safi na salama “
“Lakini
pia nisisitize kwamba tuhakikishe vyanzo vya maji vilivyopo
tunavilinda kwa nguvu zote kwani vinazidi kupungua kutokana na
uharibifu wa mazingira pia wananchi wakielimishwa wanaweza kuvitunza,
“Alisema.
Aidha aliwataka wananchi hao kuhakikisha
wanaendelea kuvitunza vyanzo vya maji ili viweze kusaidia vizazi vya
sasa na baadae kwani bila kufanya hivyo chanzo hicho kinaweza kukauka.
“Lakini kitakapokauka watu watafikiria kwenda mto Pangani
na huko kunaweza pia kukauka hivyo kuna umuhimu wa kuhakikisha vyanzo
hivyo vinatunzwa kwa lengo la kuendelea kuwepo “Alisema.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkuu wa wilaya ya Muheza
Mhandisi Mwanasha Tumbo katika taarifa yake alimueleza Waziri Mbarawa
kwamba hali ya upatikani maji wilayani humo eneo la mjini ni asilimia
35 kwa mjini na kipindi cha kiangazi asilimia 18.
Alisema
kwa upande wa vijiji upatikanaji wa maji ni asilimia 65 inakuwa ni
nafuu kwa sababu baadhi ya maeneo kuna maji yanatiririka sehemu ambazo
kumejengwa vyanzo vya maji na hivyo kuyapata kirahisi.
“Mradi wa maji eneo la Muheza mjini ulijengwa mwaka 1977 ukitumia
chanzo cha Mkurumuzi kilichopo Magoroto huku kililenga kuwapata huduma
hiyo wakazi 8000 lakini kwa sasa sasa wapo wakazi 32000.
Mkuu huyo wa wilaya alimueleza waziri huyo kwamba mpango wao kwa
sasa ni kuhakikisha wanapata chanzo cha uhakika ili kupata maji ili
kuondosha changamoto kubwa ya wilaya hiyo.
“Kwani mh
Waziri wakati wa kiangazi wananchi wananua ndoo moja ya maji kwa
sh.1000 jambo ambalo ni changamoto kubwa na hilo linaweza kupatiwa
ufumbuzi kwa miradi mikubwa “Alisema
Naye kwa upande wake
Mbunge wa Jimbo la Muheza (CCM) Balozi Adadi Rajabu alisema eneo hilo
la chanzo lilikuwa kwenye hali mbaya baada ya kuvamiwa na watu
waliokuwa wakitafuta madini kabla ya kushirikiana na watu wa maliasili
na serikali ya wilaya kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na kulirudisha
kwenye hadhi yake.
Alisema pia waliwapeleka wataalamu ili
kuangalia kama kweli kuna mamdini kwenye eno hilo ili kama wanaweza
kuruhusu uchumbaji wa madini ufanyike bila kuathiri chanzo cha maji
hivho hivyo taarifa yao bado tunaisubiri.
“Lakini pia
niwashukuru Tanga Uwasa wameanza mikakati ya kuwapa maji vijiji vyote
vinavyozunguka chanzo hicho kuhakikisha nao wananufaika na hduuma hiyo
muhimu badala ya kutumia maji yanayo tiririka “Alisema.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...