Hayo ameyasema leo Februari 22,2019 Mjini Shinyanga kwenye kikao cha Wadau wa Pamba kilichofanyika kwenye ukumbi wa SHIRECU,ambacho kimejumuisha mikoa sita ukiwemo mkoawaMwanza,Geita,Simiyu,Mara,Shinyanga na Tabora ambapo amesema ushirika wa sasa siyo kama ule wa zamani wa kupiga dili na kuongeza kuwa watahakikisha kila fedha ya vyama vya msingi inatumika ipasavyo.
Alisema suala la uchaguzi ndani ya vyama vya ushirika halina msimu na kuwataka warajisi wasaidizi wa kila mkoa kuchukua hatua haraka, iwapo kiongozi akienda kinyume na taratibu aondolewe mara moja katika nafasi yake kwani wanahitaji kuleta mabadiliko kwenye ushirika ambao utakuwa unaweza kujitegemea.
“Tunahitaji mtu anayeingia kwenye ushirika ajitathimini kwanza mwenyewe ,tunahitaji kujenga ushirika na mahali popote pale mkigundua kuna shida chukueni hatua,najua hata nyinyi viongozi kama mngekuwa na shida leo hii tusingekuwa nanyi hapa kwenye kikao hiki ninachowasihi simamieni vizuri ushirika”,alisema kaimu mrajisi.
Kwa upande wake Meneja wa Bodi ya Pamba Kanda ya Ziwa Jones Bwahama alisema changamoto kubwa waliyokumbana nayo vijijini ni baadhi ya wakulima kutonyunyizia dawa pamba yao kwa hofu kuwa itakauka kutokana na mvua kutonyesha jambo ambalo ni upotoshaji mkubwa na kuwatakakupulizia ili kuzuia wadudu wasiendelee kuharibu.
Alisema wakulima wasipopulizia viuadudu pamba inaendelea kuharibika kwani kuna wadudu wanaofyonza na wanaokula vitumba ambapo majani yanaanza kujikunja ,ambapo aliwaondoa hofu wakulima na kuwataka kupulizia pamba yao isiendelee kuharibika kwani haiwezi kukauka. Kikao hicho cha wadau wa pamba kimejumuisha warajisi wasaidizi wa mikoa,maafisa ushirika,viongozi wa vyama vya msingi na wadau wa zao la pamba,ambao wanatoka katika mikoa sita ambayo yote inajihusisha na kilimo cha pamba licha ya mikoa kufikia kwa sasa 17 lakini kikao hicho kimehusisha mikoa sita.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...