WAZIRI
wa Nchi,Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa(TAMISEMI)Sulemani Jafo amesema ndoto yake ni kuona eneo la bonde
la Mto Msimbazi jijini Dar es Salaam ambalo limekuwa kero kwa muda mrefu
sasa linaboreshwa na kuwa eneo ambalo litakuwa kivutio.
Ametoa
kauli hiyo leo Februari 25,2019 wakati anazungumza na maofisa wa ngazi
mbalimbali wa Benki ya Dunia ambao wapo nchini na leo na kesho watakuwa
kwenye ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayoendelea ndani ya Jiji
hilo ikiwemo ya miundombinu ambapo amesema Dola milioni 100 zinahitaji
kwa ajili ya kuboresha bonde hilo na hivyo ametoa ombi kwa benki hiyo.
Amefafanua
katika bonde la Mto Msimbazi zipo familia ambazo zimepoteza wapendwa
wao kutokana na kufa maji kutokana na mafaruko ambayo yamekuwa yakitokea
wakati wa msimu wa vua, hivyo anachotamani ni kuona kero iliyopo bonde
la Msimbazi inatatuliwa na kubaki eneo salama na kivutio.
"Mimi
ni Waziri ni mdogo na ukweli ndoto niliyonayo ni kuona kero ya bonde la
Mto Msimbazi inaondolewa na kubaki eneo salama ambalo litakuwa kivutio.
Dola Milioni 100 zinahitajika kukamilisha mradi wa kuboresha bonde
hilo.Ni matumaini yangu Benki ya Dunia mtashirikiana nasi kama ambavyo
tunashirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo," amesema Waziri
Jafo.
Eneo hilo la
msimbazi kupitia mradi huo wa uborshwaji wa eneo hilo litakuwa kivutio
kutokana namna ambavyo utajengwa kwa kuwa na maeneo ya kupumzika na
kubwa zaidi mandhari yake itavutia watu wengi.
Maofisa
hao wa Benki ya dunia ambao kabla ya kuanza ziara ya kutembelea miradi
ambayo wanaifadhili, walifika ofisi za TAMISEMI ambapo Waziri Jafo
ametoa shukrani kwa benki hiyo kwa namna ambavyo inatoa fedha kwa ajili
ya kufanikisha uboreshaji wa sekta mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa
miundombinu ya barabara,majiji nane,elimu,afya na sekta nyingine.
Wakati
huo huo Waziri Jafo amezungumzia namna ambavyo maeneo mengi ya nchi
yetu yameboreshwa kutokana na ushirikiano mzuri kati ya Serikali ya
Tanzania na Benki ya Dunia."Benki hii imetoa Sh.trilioni mbili kwa ajili
ya kuboresha miundombinu katika majiji nane pamoja na uboreshaji wa
maeneo mengine.
"Kwa
namna nchi yetu ilivyojenga Watanzania ambao wameondoka miaka 10
iliyopita wakirudi leo hii wanaweza kupotea kwenye baadhi ya mitaa,kwani
imeboreshwa sana.Hata yale maaneo ambayo yalikuwa hayapiti leo hii yana
barabara na yanapitika vizuri.Ukweli mitaa mingi imeboreshwa."
Amewaambia
maofisa wa Benki ya dunia kuwa Serikali ya Tanzania inatoa shukrani
nyingi kwa benki hiyo na kubwa zaidi inatambua namna ambavyo inathamini
mchango wao wa kusaidia uboreshaji wa sekta mbalimbali.
Kuhusu
ziara ya maofisa hao,amewaambia kuwa watapata fursa ya kuona namna
miradi mingi iliyotekelezwa na ile ambayo bado ipo katika hatua
mbalimbali kupitia Mradi wa Uendelezaji Jiji la Dar es Salaam(DMP).
"Mtapata
fursa za kuona namna ambavyo Jiji la Dar es Salaam lilivyoboreshwa
kupitia miradi ya DMP.Tunashukuru kwa ushirikiano wenu Benki ya
dunia,tuendelee kushirikiana.Rais wetu Dk.John Magufuli ametoa maelekezo
Makao makuu ya Serikali yawe Dodoma na Jiji la Dar es Salaam liwe la
kibiashara .Hivyo tunaka kuona Jiji hili linavutia kibiashara," amesema
Waziri Jafo.
Kwa upande
wao maofisa wa Benki ya Dunia wamemwambia Waziri Jafo kuwa
wamefurahishwa na namna ambavyo utekelezaji wa miradi hiyo na kwamba
wataendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuhakikisha wanaendelea
kusaidia fedha za miradi ya maendele



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...