Ndugu Wanahabari, mimi ni Philipo Mwakibinga mwanachama wa kawaida wa CCM niliyetokea upinzani. Kama mnakumbukumbu mwaka wa jana mimi ni mmoja wa watu ambao kwa dhamira zao bila shurti tuliachana na siasa za upinzani za majitaka na ghiriba kisha kujiunga na CCM ili kupata fulsa ya kujenga taifa kwa bila ubabaishaji wowote.
Na ikumbukwe kuwa sote tuliotoka huko hakuna hata mmoja aliyesifia upinzani bali tuliuponda na kuanika hadharani maovu ya upinzani na hasa mifumo mibovu na ombwe la uongozi ambapo hadi sasa vyama vya upinzani havijabadirika bado ni vibovu vinazidi kudorora kila kukicha.
Ndugu wanahabari, nimejitokeza kuongea nanyi baada ya kusikia taarifa iliyoandaliwa na CHADEMA kisha kutolewa na mtu anayejulikana kwa jina la KIDERA. Kidera ametoa kauli huku akiwa chini ya ulinzi wa viongozi wa CHADEMA na akiwa kama mateka wa kisiasa.
Hivyo kwa yale yote aliyoyasema nimeona nivyema na nibora sana mimi kama Mwanachama wa kawaida kabisa ndani ya CCM tena nikiwa nimetoka huko upinzani nisikae kimya na kuacha uongo, na uzushi ukatamalaki. Nasema wazi kuwa kinachofanywa sasa ni mkakati wa hovyo wenye nia ovu unaofanywa na CHADEMA na mawakala wao katika kukengeusha Demokrasia tulivu inayosifiwa Ulimwenguni kote iliyopo ndani ya Taifa letu.
Ndugu Wanahabari nivyema nikafafanua mambo yafuatayo:
Suala la Kwanza: KUNATOFAUTI KUBWA KATI YA CCM NA UPINZANI.
CCM ni chama kinachoongozwa na, Kanuni, taratibu na miongozo. Hii haipo katika chama chochote cha Upinzani. Huko kwa wenzetu ambako siye tumekulia Kanuni, taratibu na miongozo vipo kwenye nguvu za mtu mmoja tu. Mfano CHADEMA kila jambo lipo katika hatima ya mikono ya Kiongozi mmoja. Hivyo mtu anapotoka CCM nakurudi huko jua kashindwa kuishi kwa kanuni, taratibu na miongozo bali anapenda kuishi kihovyo hovyo.
Hii ni hatari sana na kwenye chama cha upinzani ukifanya mambo ya hovyo ndiyo unakua maarufu kwani unakua umewakosha wahovyo wenzio. Utaitwa Kamanda, Mzalendo na majina mengi ya namna hiyo. Uhovyo wa namna hiyo CCM haupo kabisa na, ukizoea ujinga huo huwezi kuishi CCM utaondoka kama KIDELA maana utaona kama unatengwa maana kila mmoja yupo busy kutatua changamoto za jamii.
Suala la Pili: UTARATIBU NA MFUMO WA UONGOZI NDANI YA CCM UNAELEWEKA: Ndani ya CCM upatikanaji wa uongozi kwa nafasi za kugombea ni kila baada ya miaka mitano. Hivyo kama uchaguzi umefanyika na hukupata nafasi inabidi uungemkono waliochaguliwa kwaajili ya kufanya kazi ya Chama na Taifa kwa ujamla hii ndiyo demokrasia yenye misingi ya haki na usawa.
Isipokua nafasi za kuteuliwa hizi hupatikana kulingana na matakwa ya kanuni, taratibu na mahitaji ya mamlaka za uteuzi kwa mujibu wa miongozo. Hivyo waliokosa nafasi kama bado wanahitaji kupata nafasi za kugombea lazima usubiri baada ya kipindi hicho tajwa hapo juu. HIVYO CCM NDICHO CHAMA CHENYE KATIBA BORA ZAIDI YENYE KUZINGATIA DEMOKRASIA PANA. Sasa KIDERA anatoka CHADEMA anataka uchaguzi ufanyike ili kupata madaraka kwasababu tu kahamia.
Hakuna demokrasia ya namna hiyo huku CCM hayo yapo CHADEMA ndiyo maana kuna nafasi hazieleweki zinapatikanaje kwani ni chama kisicho na misingi inayoeleweka ni kikundi tu bora hata SACCOS zina utaratibu fulani kwa wakopaji wake lakini hawa wenzetu wako hivyo mnavyowaoana. KIDERA alipaswa kufanya tafiti kwanza juu ya CCM kabla hajahamia na kushindwa kufanya hivyo ni wazi kajianika kuwa mtu asiye makini na hii ni dalili mbovu kwa wanasiasa wa aina ya KIDERA maana hawana mapenzi ya kweli na Demokrasia bali wanakua wanaajenda binafsi tofauti na malengo madhubuti ya chama cha siasa.
Suala la Tatu: UAMINIFU WA KIDERA UNATIA MASHAKA HATA KWA HISTORIA YAKE:
Kidera ni kijana mwenye tamaa. Hata Chadema wanamjua vizuri amekua mtu mwenye kuendekeza tamaa ya madaraka kwa muda sasa. Hili linatokana na yeye kufanya siasa huku akiwa hana kazi nyingine yoyote ya kufanya. Hivyo anachofanya ni kulazimisha siasa iwe sehemu ya kupata mkate wake wa kila siku. Nakumbuka tulipokua ukonga kwenye uchaguzi mdogo alipohamia CCM aliwahi kuja na bajeti ya kiasi cha shilingi milioni 10 aliyoiandaa chumbani kwake ili apewe pesa akidai anavijana watasaidia kuleta siri za CHADEMA.
Kila mmoja alimshangaa alipoambiwa hakuna CCM ya hivyo na kuona amepuuzwa ndiyo akaanza kupika majungu na kwenda kuramba nyayo hao waliomfuga ili arudi kama alivyofanya. Undumila kuwili alionao ni hatari sana katika hatma yake ya kisiasa. Kidera huyu ndiye yule Aliyegombea kura za maoni ndani ya Chadema aliposhindwa akaanza kuwachafua viongozi wake ndiye aliyeleta migogoro ya UKAWA huko Segerea kama mnakumbuka.
Nao CHADEMA kwasababu ya kuleana kizembe wakampa uenyekiti wa jimbo akatulia kidogo. Ulipofika uchaguzi wa Serikali za Mitaa akagombea Uenyekiti wa Mtaa na alipopata tu alitumia nafasi hiyo kujipatia pesa zile ndogo ndogo baada ya kurubuni watu huko wakisuruhisha migogoro.
Hayuko safi hata kidogo. Rekodi yake tu inamfanya akose uhalali wa kuzungumza hata mbele ya wenye akili za kupambanua mambo. Sasa alipohamia CCM kwa kuamini yeye ni mtu muhimu kwahiyo atapata cheo kikubwa zaidi ndiyo njaa imemshika sasa kakoma kwa tamaa yake ya Fisi.
Anasema kuna viongozi walimuahidi madaraka kama siyo upungufu wa ufikiri kichwani unawezaje kuahidiwa madaraka yasiyo kuwepo na wewe ukaamini? Hakuna jambo hilo ni mwamvuli tu mbovu wanatumia na wenzake hao ilikujificha wakitaka kuhalalisha uongo wao. Huyu ni mpiga dili tu wa kisiasa ambaye kashindwa kuvumilia CCM maana huku unapaswa kuwa na kazi inayokupa kipato na ndipo ushiriki siasa.
Suala la Nne: CCM ni chama bora zaidi barani Afrika. Ndicho chama cha ukombozi kinachotoa dira ya maendeleo. Mtakumbuka Prof. Lumumba wa Kenya alitaja vyama viwili tu vinavyostahili kubaki barani Afrika katika vyama hivi CCM moja wapo. Sasa asije mtu yeyote akachukulia poa na kufikiri ni chama cha mchezo huyu atajikuta yuko peke yake. Sehemu pekee ya kufanya siasa za mchezo, masiara na kupoteza muda ni huko upinzani walikozoea ambako nirahisi kupeana umaarufu wa ajabu kwa sababu ya mambo ya hovyo. CCM imepewa mamlaka na Wananchi kwasababu inamipango endelevu.
Hivyo KIDERA anaposema haoni mazingira ya kufanya siasa akiwa ndani ya CCM niwazi hajui maana ya Siasa. Atambue kuwa CCM inaamini kuwa SIASA NI MAENDELEO na siyo makelele yasiyo na masingi. Kajidhalilisha kwani kakimbia siasa ya maendeleo na kwenda kwenye siasa ya makelele, kupinga kila kitu na kulalama pasipo kuwa majibu na suluhu za matatizo ya jamii.
Suala la Tano: kutokana na mfumo bora wa CCM ndiyo maana chama hiki kimetoa RAIS BORA ZAIDI BARANI AFRIKA. Ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM. Ninyi ni mashahidi mmeona namna anavyopokelewa na kuhitajika kwenye mataifa ya wenzetu. Tumeona Alipokwenda S.Afrika, Namibia na Zimbabwe. Mapokezi aliyoyapata na namna anavyoheshimika sana. Hii ni alama kubwa na tunu kwa Taifa letu.
SUALA LA SITA: NAWAONYA Viongozi wa CHADEMA hasa Bonphace Jackob kuacha kuacha upotoshaji wa makusudi wakati wanajua kabisa KIDERA si mwenzao siku nyingi. Bonphace anajua kabisa namna KIDERA alivyotoka na kurudi ndani ya CHADEMA vikao vyote mlivyokuwa mnakaa na namna alivyokuwa anawasiliana na ninyi tunajua. Sasa kuhadaa UMMA kwamba CCM hakuna mazingira ya safi ya kufanya Sisa wakati KIDERA huyo ndiye aliyeeleza watu wa UKONGA kwenye kampeni mambo yote maovu ya CHADEMA na VIONGOZI wake akiwemo huyo BONPHACE.
HIVYO: Natoa Rai kwamba wale wote walio hamia CCM kwa kufuata mkumbo, kusaka madaraka na kufikiri atapata nafuu ya kubebwa ni Bora watoke warudi huko walikozoea upuuzi wa namna hiyo. CCM ni kazi, Uzalendo uliotukuka, na sehemu ya kuwa mtumishi wa umma. CCM ni uadilifu malengo ya kitaifa na kuwa majibu sahihi ya maswali ya jamii. Tuwapuuze wale wote wasio na hekima kwani wamebembendwa kisiasa huko walikotoka wanataka kuendekeza udumavu wa kisiasa. Wale tuliohamia kwasababu ya kulipenda taifa na kuamini kazi inayofanywa na CCM na viongozi wake kupitia mwenyekiti ambaye ndiye Rais wa Nchi basi tuendelee kuchapa kazi na kuwa majibu sahihi ya matatizo ya Watu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...