Afisa Biashara
Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kati kati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa
mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Mkuu wa Kitengo, Idara ya Huduma za Masoko William Mpinga na kulia ni Balozi
wa kampeni hiyo Lucas Muhavile maarufu kama Joti.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga (kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama
‘Saizi Yako‘ uliofanyika jijini Dar es Salaam. Katikati ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf akifuatiwa na Balozi wa kampeni hiyo Lucas Muhavile
maarufu kama Joti
Balozi wa Kampeni mpya ya Tigo
inayojulikana kama ‘Saizi Yako’ Lucas Muhavile maarufu kama ‘Joti’ akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ofa hiyo
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Afisa Biashara Mkuu Tigo Tarik Boudiaf na William Mpinga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za
Masoko wa kampuni hiyo.
Afisa Biashara
Mkuu wa kampuni ya Tigo Tarik Boudiaf(kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na mchekeshaji Lucas Muhavile maarufu kama Joti (kati
kati) Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko wa kampuni ya Tigo William Mpinga
muda mfupi baada ya uzinduzi wa ofa mpya inayojulikana kama ‘Saizi Yako‘ uliofanyika
jijini Dar es Salaam.
Wateja wa Tigo sasa wana kila sababu ya kufurahi baada ya uzinduzi wa ofa mpya ya ‘Saizi Yako’ inayolenga kuwapatia huduma za intaneti, muda wa maongezi na SMS kutokana na mahitaji mahususi ya kila mteja kwa gharama nafuu.
Ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ni ya kipekee sana kwa sababu inawapatia wateja ambazo ni mahususi kwa kila mteja hivyo kuwaridhisha wateja wa sasa na wa baadaye wakiangalia gharama wanayoitumia kulinganisha na huduma wanayoipata. Ofa hii pia inapatikana kupitia menyu iliyorahisishwa ili wateja waweze kuipata na kuinunua kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa ofa hii kutoka makao makuu ya Tigo, Dar es Salaam, Afisa Biashara Mkuu wa Tigo, Tarik Boudiaf, alisema kwamba lengo la kampuni hiyo ni kutoa ofa bora, zenye mahitaji yote ya mteja sehemu moja, kwa gharama nafuu, na zitakazo kidhi mapendekezo na mahitaji ya wateja wao.
“Tumezingatia tabia, mahitaji na mienendo ya wateja wetu kwa miaka mingi sasa. Na kinachotufanya tuwe wabunifu ni kwamba tunatambua kwamba kila mteja wetu ni wa kipekee. Hivyo, tumeamua kubuni ofa hii ya ‘Saizi Yako’ ambayo ina mahitaji yote ya mteja sehemu moja na inayozingatia mahitaji yao mahususi. Sasa tunatoa fursa kwa wateja wetu kuweza kupata ofa za kipekee kwa kuzingatia matumizi yao ya kila siku na kwa gharama nafuu,” alisema Boudiaf.
Boudiaf pia alieleza kwamba, kama mteja anatumia muda wa maongezi zaidi kuliko intaneti na SMS, basi atapata kifurushi bora cha muda wa maongezi. Na mteja akitumia zaidi intanet kuliko muda wa maongezi na SMS, mteja huyo atazawadiwa kifurushi bora cha intanet. Utaratibu huo huo utafuatwa pia kwa ajili ya SMS.
“Tunaamini kwamba ‘Saizi Yako’ itaendana na mahitaji, bajeti na maisha ya wateja wetu. Kuwapatia ofa ambayo wataweza kupata kila wanachohitaji sehemu moja, kwa ajili yao, pia inamaanisha kwamba, sisi kama Tigo, tunatambua na kufanyia kazi mahitaji ya wateja wetu yanayobadilika kila siku. Uelewa wetu wa wateja pia unajenga mahusiano yetu nao na kuwafanya watuthamini zaidi,” aliongeza Boudiaf.
Kufurahia ofa maalumu ya ‘Saizi Yako’, wateja wanaweza wakapiga *147*00# au *148*00# kwa urahisi na kuchagua ‘Saizi Yako’. Ofa hii pia itapatakina katika Tigo Pesa APP hivi karibuni.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...