Kocha wa timu ya taifa Taifa Stars Emmanuel Amuneke, ana matumaini kuwa bado timu yake ina nafasi ya kufanya vizuri katika mchezo wa tatu wa mashindano ya Mataifa Afrika dhidi ya Algeria,utakaofanyika Julai 1,katika Uwanja wa Al- Salam nchini Misri.
Akizungumza na waandishi wa habari,Amuneke,alisema kuwa licha ya kuwa Algeria ina kikosi kizuri,lakini bado ana matumaini makubwa na vijana wake kuwa watafanya vizuri katika mchezo huo wa mwisho wa kundi C.
“Tumecheza na Algeria mara kadhaa,nakumbuka mchezo wa Dar es Salaam tuliocheza tukafungwa bao mbili kwa sifuri,na baadaye tukaja kucheza nao tukatoka nao 2-2,nakumbuka pia walikuja wakatufunga bao 7 kwa bila,lakini hiyo yote ni historia,”alisema na kuongeza:
“Kwasasa hivi tunachokitazama ni namna gani tutaweza kusawazisha makosa yetu yaliyotokea katika michezo miwili iliyopita,na kufanya maamuzi sahihi tunapokuwa na mpira,kwahiyo Jumatatu ni ukurasa mwingine na ni safari nyingine kwa Tanzania na Algeria,na hauwezi kutabiri nani atakuwa mshindi,kwahiyo tutaingia uwanjani kupambana na kusaka pointi tatu.”
Taifa stars,itashuka dimbani kupambana na Algeria baada ya kupoteza mchezo wa awali dhidi ya Senegal kwa bao 2-0 na mchezo wa pili dhidi ya Kenya ulioisha kwa Kenya kuibuka na ushindi wa bao 3-2.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...