Na,Vero Ignatus Arusha.
Halmashauri
Kuu ya mkoa wa Arusha CCM imepokea Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya
CCM 2015-2020 Kwa kipindi cha Robo Tatu ya Mwaka wa Fedha Julai-March
2019.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Kikao hicho Katibu mkuu wa CCM mkoa Mussa Matoroka
amesema kuwa kabla ya kufanya kikao hicho walifanya ziara katika wilaya
zote zilizopo mkoani humo kukagua shughuli za maendeleo na kujiridhisha.
Mrisho
Gambo amesema kuwa hali halisi ya mapato katika mkoa huu ni ndogo
ukilinganisha na matumizi kwa mwaka huku akisema kuwa serikali kuu
imekuwa ikiibeba mkoa ili kukukidhi mishahara ya wafanyakazi mkoani
humu.
Aidha amesema
serikali imefanya mambo mengi Sana katika mkoa huu Kama za ujenzi wa
barabara za lami na sisizo za lami huku, kujenga madaraja ya kiwango
kizuri ili kurahisha huduma za kijamii pamoja na upatikanaji wa mkoani
maji ya kutoka mkoani hapa.
Aidha
amesema kuwa Serikali kwa nguvu kubwa imeweka nguvu kubwa katika
kujenga barabara la lami yenye kilimita 49 Wilayani Ngorongoro jambo
ambalo halijawahi kufanyika tangu uhuru wa Tanzania bara.
Katika
uwasilishaji huu, Mrisho Gambo amesema kuwa Serikali pia imewezesha
upatikanaji wa maji ya kutosha kwa asilimia mia moja pindi mradi
utakapokamilika na wanachi wote mkoa ni watapata maji safi na salama
ukilinganisha na asilimia 40 ya maji
yanayopatikana kwa sasa.
Kuhusu
huduma za afya, Mrisho Gambo amesema ametoa fedha za kujenga hospitali
za Wilaya katika zote mkoani Arusha hivyo kufanya Kila wilaya kuwa na
hospitali yake huku akisema kuwa bado serikali imejenga vituo vipya vya
afya katika mkoa mzima wa Arusha.
Aidha
Gambo amewataka viongozi wa dini kuendelea kuiombea na nchi na
kudumisha na kuhubiri Amani katika ibada zao kwani ikiondoka hakuna
atayeweza kuirejesha Ameongeza
kuwa miradi hiyo inayosimimamiwa na kutekelezwa na Serikali haijapata
msaada wowote toka nje, amesema yote ni mapato na makusanyo ya ndani.
Naye
kamishna Msaidizi wa Mkoa wa Arusha Jonathan Shani amesema kuwa katika
kutekeleza ilani ya CCM, Jeshi la Polisi mkoani hapa wanatekeleza kwa
kudumisha ulinzi na Usalama kama jina lijulikanavyo la Geneva of Africa.
Aidha
ametoa onyo kali kwa watakaojaribu kuhamasisha ama kujaribu kuandama
huku akisema kuwa wanaendelea kuhakikisha Arusha itakuwa mbali na madawa
ya kulevya.
Ameongeza
kuwa Jeshi la Polisi lipo kuwalinda wananchi wote ila akatoa wito kwa
kwa wanawake kuwa ulinzi upo kwao na Kila atakayemtesa mwanamke
atachukuliwa hatua stahiki kwa wanaowanyanyasa wake zao.
Hata
hivyo kamanda huyo amesema kuwa ulinzi katika mkoa wa Arusha na mipaka
yake upo imara na kwamba wananchi wote wasiwe na shaka




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...