Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
Kasi ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari, Rais Dkt. John Pombe Magufuli imewavutia Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza Ilani yake ya Chama kama ilivyoahidi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), Ujenzi wa Uwanja wa Ndege (Terminal 3), Ujenzi wa Barabara (Daraja la Mfugale, Ubungo Interchange), pamona na Bandari Kavu. 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wajumbe hao wakati wakitembelea miradi hiyo katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na Pwani wakiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM),Humphrey Polepole, Mmoja wa Wajumbe wa Kamati hiyo, Livingstone Lusinde amesema wanampongeza Mhe. Rais na Serikali yake yote kwa kasi anayoionyesha.

"Wale ambao hawajaona maendeleo haya wasubiri kuona, anayebeza mambo haya sio mzalendo, ni mtu ambaye hajui maana ya maendeleo", amesema Lusinde.

Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba amesema maendeleo yanayoonekana sasa hivi ni jambo lakujivunia kwa Taifa zima kwa Mhe. Rais chini ya Serikali ya awamu ya tano kutekeleza mambo yote yakimaendeleo.

"Kwa nchi za Afrika Mashariki tunajivunia Uwanja mkubwa wa Ndege, tunayaona maendeleo kwa kweli wale waliokuwa wanasema hakuna maendeleo wana sababu zao, siku zote mwenye macho haambiwi tazama", amesema Kate Kamba.

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika picha ya moja mara baada ya kukaguwa  ujenzi wa daraja linalokatiza baharini na kuunganisha maeneo ya Aga Khan na Coco Beach Jijini Dar es Salaam. Daraja hilo limependekezwa kuitwa Tanzanite Bridge.      

 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRC) Masanja Kadogosa (kulia) akitoa maelezo kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM)   wakati alipotembelea ujenzi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali jana juni 26,2019.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa juu ya daraja Mfugale, katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali leo juni 26,2019.
 Msimamizi wa jengo la tatu la abiria kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere,Mhandisi Barton  Komba akitoa  maelezo kwa wajumbe wa Halmashauri kuu Taifa  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali jana juni 26,2019.
 Mataaluma yakiwa tayari kwenye kiwanda cha kilichopo Soga mkoa wa Pwani kwaajili ya kwenda kuwekwa kwenye maeneo ambayo reli ya kisasa itapita.
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kiwanda Mataaluma Soga mkoa wa Pwani.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Mchuzi Tv)

Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakikaguwa ujenzi wa shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo mkoa wa Pwani.
  Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa  Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiendelea na ukaguzi wa jengo la tatu la abiria  kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere jana  juni 26,2019  katika ziara ya kukagua miranda mbalimbali inayotekelezwa na serikali.(Picha zote Emmanuel Massaka wa Mchuzi Tv)

Mafundi wakiendelea na kazi katika mradi wa reli ya kisasa ya standarge gaurge
Muonekano wa jengo la tatu la abiria kiwanja cha ndege cha kimataifa Julius Nyerere.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...