Na Jusline Marco:Arusha
JESHI la Polisi mkoani Arusha limefanyika kukamata madini aina nane yenye thamani ya Sh. milioni 958 yaliyokuwa yakitoroshwa mpakani mwa Tanzania na nchi jirani ya Kenya katika eneo la Namang.
Akizungumza leo na vyombo vya habari wakati akikabidhi madini hayo kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)kwa ajili ya kuhifadhiwa,Waziri wa Madini Dotto Biteko ameliagiza Jeshi la polisi kuwafikisha watuhumiwa wote kwenye mikono ya dola.
Aidha Waziri Biteko ameagiza vyombo vyote ambavyo vinasimamia haki sheria ichukukuwe mkondo wake ili iwe mfano kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Pia ameongeza wajibu wake na wajibu wa Serikali ni kumlinda mwananchi ambaye anafanyakazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha yule ambaye hatekelezi sheria,sheria iwezekuchukua mkondo wake dhidi.
Awali akizungumza,Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema utokewaji wa vibali kwa wafanyabiashara wa madini nchini na uwepo wa masoko ya uhakika ni ili kuwapa unafuu na kuondoa urasimu katika ufanyaji wa biashara zao.
Amesema pamoja na uondolewaji wa tozo hizo katika sekta ya madini anashangazwa kuwepo kwa baadhi ya watu wasio waaminifu katika sekta hiyo na kuisababishia serikali hasara ya mamilioni ambapo amesema kuwa ni lazima mahakama ziungane na serikali kulinda rasilimali za umma kwa kuhakikisha inatolewa adhabu kali kwa wa watu hao ili iwe fundisho kwa wafanyabiashara wenye tabia kama hizo.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoani hapa Jonathan Shanna amesema kuwa ukamatwaji wa utoroshwaji wa madini hayo ni kutokana na taarifa iliyotolewa na raia mwema ambapo saa tisa ya usiku wa kuamkia leo Jeshi la Polisi walifanikiwa kuwakamata watu watatu waliokuwa wakisafirisha madini hayo.
Amewataka watuhumiwa hao ni Joseph Abdallah(41), aliyekuwa dereva wa basi la abiria la Perfect namba T 716 AAC ,Kondokta Mohamed Madume (36) na Latifa Abdallah(42) mkazi wa Sakina ambaye ndio mwenye mzigo huo na wote ni wakazi wa Arusha.
Waziri wa madini Dotto Biteko wa kwanza kulia akikagua madini yaliyokuwa yamehifadhiwa benki kuu Mkoani Arusha baada ya kukamatwa jana mpakani mwa longido na nchi jirani ya Kenya
Waziri Biteko akihakikisha madini hayo tayari kwa kuhifadhiwa katika ghala maalum la Benki kuu,wa kwanza kulia ni Gavana Mkazi Benki Kuu tawi la Arusha Charles Yamo




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...