Na Woinde Shizza Michuzi Tv,Arusha

Jamii imetakiwa kuhamasisha watoto wao kupenda kujisomea vitabu mbalimbali kwenye Maktaba ili kuepuka vishawishi na matendo yasiyofaa ikiwemo kuvuta bangi na ubakaji.

Kauli hiyo imetolewa jana na Mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqqaro wakati alipokuwa akizindua kituo kipya cha Maktaba ya Jamii cha Madecha kilichojengwa katika Kata ya Sinoni kwa thamani ya zaidi ya sh, Mil.40 chini ya ufadhili wa familia ya Mathew Hladezuk(17) kutoka nchini Marekeni.

Akizungumza katika hafla hiyo,mkuu huyo wa wilaya ,mbali na kumpongeza mwanzilishi wa kituo hicho,Profesa Richard Msomba na Mkewe Elaine Msomba alisema ipo haja kwa kila mzazi kumhamasisha mtoto wake kujisomea vitabu mbalimbali katika Maktaba hiyo jambo litakalosaidia kuongeza uelewa katika masomo yao.

"Vijana wa kata ya Sinoni watumie Maktaba hii kujiendeleza kielimu na serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ,kwani vijana wetu wakihamasika vizuri kujisomea itapunguza matukio ya uhalifu" Alisema Daqqaro

Awali mwanzilishi wa Maktaba hiyo,Prof,Richard Msomba ambaye ni mwalimu wa uchumi nchini Marekani alisema kituo hilo kitakachohudumia bure wanafunzi wa Chekechea hadi kidato cha Sita.

Alisema ameamua kujenga Maktaba hiyo yeye na mke wake,Elaine Msomba kama sehemu ya mchango wao kwa jamii katika kuendeleza sekta ya elimu baada ya kubaini kuwa Jamii haina Huduma hiyo na watoto wengi wanajisomea majumbali mwao na kukosa sehemu ya utulivu. .

"Maktaba hii itahudumia shule mbalimbali za sekondari na msingi zipatazo 17 na wanafunzi wapatao 140 wanajisomea kwa kila siku na wakati wa mitihani wanafunzi wanakuwa wengi zaidi" Alisema prof.Msomba.

Aliongeza kuwa changamoto kubwa walionayo wanafunzi ni uwezo wa kununua vitabu hivyo wamewasogezea Huduma ya vitabu na watakuwa wanajisomea bure bila kulipa gharama yeyote.


Aliiomba Jamii kuwa na Moyo wa kujitolea kuisaidia Jamii isiyona uwezo kama ambavyo yeye amefanya kwa kuanzisha kituo hicho cha Maktaba ya Jamii.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo,Godfrey Simbile àliishuuru familia hiyo kwa kuwaletea karibu Maktaba hiyo katika Kata yake na kueleza kuwa jukumu lake ni kuhakikisha wananchi wake hususani vijana wanahamasika kuja kujisomea katika Maktaba hiyo.


"Maktaba hii itasaidia watoto kujiendeleza kielimu kupitia vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika maktaba hii na itapunguza matukio ya uhalifu na vishawishi vibaya.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro(kati) akizungumza katika uzinduzi wa kituo cha maktaba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...