Mgeni Rasmi ambaye ni Mhariri Mkuu wa kampuni ya Tan Communication Media wamiliki wa Redio 5 Arusha,Bi.Ashura Mohamed akizungumza na wachezaji wakati wa uzinduzi rasmi wa michezo hiyo.
Robert Pius Afisa Michezo 977 akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Tanganyika uliopo Jijini Arusha

Mratibu wa mashindano hayo ambaye ni mdau wa michezo Bw.Benjamini Mathayo akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na Mashundano hayo ya Ndondo Cup
Timu mbili zilizocheza wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo Timu ya Jeshi kikosi cha 977 Upendo Fc ambapo timu ya Kikosi cha Jeshi 977 iliibuka mshindi katika mechi hiyo ya Ufunguzi kwa Kuichapa Upendo Fc goli 4-0.
Mgeni rasmi Bi Ashura Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na Timu ya Jeshi kikosi cha 977 Upendo Fc.
Mgeni rasmi Bi Ashura Mohamed akiwa katika picha ya pamoja na Timu Upendo FC
Na.Vero Ignatus,Arusha.
Mashindano ya Jumuiya ya Michezo Arusha maarufu kama (Arusha ndondo Cup) yamefunguliwa rasmi jana katika Viwanja vya Jeshi kikosi cha 977 Tanganyika pekas,ambapo Jumla ya timu 20 kuchuana hapo.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo Bi.Ashura Mohamed kutoka ya Tan Communication Media wamiliki wa Redio 5 aliwataka vijana hao kuchukulia Mashindano hayo kama chachu ya kuendeleza Vipaji vyao.
Alisema kuwa mchezo wa soka hapa nchini na duniani ni mchezo wenye mashabiki wengi hivyo waendelee kufanya mazoezi kwa bidii na kuwa na nidhamu ili kukuza vipaji na kutumia mashindano hayo Vyema kujitangaza.
Aidha aliwataka marefa ambao wanachezesha mechi zote pamoja na waratibu wa mashindano hayo kuhakikisha kuwa wanatumia sheria kumi na saba za mpira wa Miguu ili kuhakikisha kuwa Mshindi halali anapatikana badala ya kubebana.
“Nimeelezwa kuwa mashindano haya yameanza mwaka 2015,yakiwa na timu 12 leo tuna timu 20 ni hatua nzuri na inaonesha wazi kuwa mmejipanga vizuri nisisitize tu sheria zifuatwe na umati huu wa watu unaonesha nia njema ya kuvutiwa na mashindano haya”Alisema Ashura.
Hata hivyo alisema kuwa ili kuongeza nguvu katika mashindano hayo ataongeza zawadi ili kuongeza hamasa kwa timu zitakazoshiriki na kufanya vyema zaidi.
Naye Mratibu wa mashindano hayo ambaye ni mdau wa michezo kutoka wilaya ya Arumeru Bw.Benjamini Mathayo alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ni kukosekana kwa vifaa vya kutosha pamoja na changamoto ya fedha hali inayopelekea kukosekana kwa zawadi za washindi pamoja na kukosa mdhamini.
Bw.Mathayo alisema kuwa mafanikio katika mashindano hayo ni kupunguza Idadi ya Matukio ya Uhalifu na utumiaji mbaya wa madawa ya kulevya.
alisema kuwa Mashindano hayo yataenda sambamba na Utunzaji wa Mazingira ambapo kila Jumapili timu zote zitapata fursa ya kupanda miti,katika maeneo ya wazi.
katika mashindano hayo timu ya Jeshi kikosi cha 977 kiliibuka mshindi katika mechi hiyo ya Ufunguzi kwa Kuichapa Upendo Fc goli 4-0.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...