Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Dar es Salaam

Imeelezwa Michepuko ndio chanzo Cha kuongezeka migogoro ya kifamilia ambapo kuanzia March 2018/2019 Mashauri ya ndoa 16832 yalipokelewa        
Kulinganisha na Mashauri 13,382 yaliyolipotiwa 2017/18

Hayo yamesemwa na Muwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr.Naftar .B. Ng'ondi Kamishna ustawi wa Jamii katika mafunzo ya agenda ya kitaifa ya wajibu wa wazazi /walezi katika malezi na matunzo ya familia Nchini Tanzania

Dr.Naftar amesema changamoto za kukithiri vitendo vya ukatili dhidi ya Watoto na wanawake,imezidi kuongezeka kwa kiasi kikubwa  kutokana na kukithiri kwa mmong'onyoko wa maadili kwa wanafamilia.

"Kwa mujibu wa takwimu za wizara ya Afya Ofisi ya Kamishna wa Ustawi wa Jamii kwa miezi Tisa kuanzia julai 2018 hadi Machi 2019 Mashauri ya migogoro ya ndoa 16832 ilipokelewa kulinganisha namashauri 13,382 mwaka 2017/18"Amesema  Dr Naftar.

Amesema migogoro hiyo inaathiri ukuaji wa Watoto , ustawi na Maendeleo ya familia,kiuchumi husababisha wanafamilia kusahau wajibu wao kwa familia .

Anataja kuwa kwa mujibu wa matokeo ya ukatili wa taarifa za Jeshi la Polisi nchini kwa mwaka 2018 matokeo ya ukatili 14,419 yameripotiwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 7.7 ya vitendo vya ukatili kwa Watoto nchini 

"ikiwemo ubakaji ,5,557,mimba 2,692,kulawiti 1,159,shambulio 965 na kujeruhi 705 huku mikoa inayoongoza ni Tanga,Mbeya , Mwanza,Arusha na Tabora"

Amesema kuwa mikoa ya kipolisi yenye takwimu kubwa za ukatili ni Kinondoni (2,426),Dodoma(1283),Tanga 1064,Temeke 984 na Arusha 972.

Amesema ni muhimu kujikumbusha na kujengeana uwezo kuhusu malezi Bora,kuboresha mawasiliano katika familia kama njia ya kutambua changamoto zinazowakabili Watoto na wanafamilia wote ili kuzitafutia ufumbuzi mapema.
Kamishna ustawi wa Jamii Dr.Naftar Ng'ondi akizungumza na Waandishi pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.
 Waandishi na wahariri wanaoshiriki mafunzo hayo

 Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya Mwelinde Kato akionesha kitini Cha muongozo was malezi kwa familia
 Mwajuma Magwiza Mkurugenzi idara ya Maendeleo ya Jamii akizungumza na Waandishi pamoja na wahariri wa vyombo mbalimbali vya Habari jijini Dar es Salaam

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...