
*Asema wanawafuatilia watumishi kwa karibu, watakaoabinika kukiona
*Waziri Mkuchika aitaja mikoa inayoongozwa kwa dawa za kulevya nchini
Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii
MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (TAKUKURU) Diwani Athumani amewataka Watanzania kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya huku akifafanua iwapo jamii ikaachwa itumie dawa za kulevya hatari zake ni nyingi ikiwemo ya uchumi kudorora na usalama wa nchi kuwa mashakani.
Akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Dawa za Kulevya Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika Jiji la Tanga, Athumani amesema tatizo la dawa za kulevya lilikuwa kubwa lakini Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imefanya kazi kubwa kukomesha biashara ya dawa za kulevya nchini.
"Ni vema Watanzania wote tukaunga mkono mapambano dhidi ya dawa za kulevya na sio kuiachia mamlaka peke yake.Nguvu kazi kubwa ya Taifa ikiendelea kutumia dawa za kulevya maana yake uchumi utadorola na kwenda kuathiri uchumi wa nchi.Pia kundi kubwa likiachwa na kuingia kwenye dawa za kulevya usalama wa nchi unakuwa shakani,"amesema Diwani Athumani.
Akifafanua zaidi kuhusu ushiriki wa TAKUKURU kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini amesema rushwa inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kukwamisha mapambano dhidi ya dawa hizo na kufafanua iwapo rushwa ikatumika mipakani maana yake wafanyabiashara hiyo watumia rushwa kuingiza dawa nchini.
"Rushwa ikiachwa na kutumika katika kupambana na dawa za kulevya maana yake ni kwamba dawa zitaendelea kuingizwa nchini na madhara yake ni kuathiri jamii katika nyanja mbalimbali.Ndio maana TAKUKURU tuko kila mahali kuhakisha hakuna rushwa katika kukomesha dawa za kulevya nchini,amesema Athumani na kufafanua Watanzania wanalo jukumu la kukemea dawa za kulevya na rushwa.
Ametoa rai kwa watumishi wote wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na dawa za kulevya kuhakikisha wanachukua rushwa katika utendaji wa kazi zao za kila siku na kwamba TAKUKURU iko kila mahali itaendelea kufuatilia na atakayepatikana ajue amepatikana.
Pia amewaomba viongozi wa dini kutumia karama ambazo wamepa na Mungu kuhakikisha wanaendelea kukumbusha waumini wao kuhusu madhara ya dawa za kulevya na rushwa katika nchi yetu kwani viongozi wa dini wanao mchango mkubwa katika harakati za kukomesha dawa hizo.
Kwa upande wake Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalim amesema watanzania lazima wachukue dawa za kulevya nchini kwani madhara yake ni makubwa huku akifafanua kwa wale ambao wameatherik na utumiaji wa dawa hizo Serikali inayo wajibu wa kuwatibu na ndio maana kuna vituo vya kutoa huduma katika maeneo mbalimbali nchini na siku za karibuni kitajengwa kituo kingine katika jiji la Tanga.
"Katika nchi yetu tatizo la dawa za kulevya linashushulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.Nitoe pongezi kwa Rais Dk.John Magufuli kwa uamuzi wake wa kukabiliana kwa vitendo na biashara ya dawa za kulevya kwa kuanzisha mamlaka hii ambayo inafanya kazi nzuri.Na tangu kuanzishwa kwa mamlaka kumewepo na ushirikiano mzuri kwa mihilimi yote mitatu katika nchi.
Wakati huo huo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma George Mkuchika akizungumza kwa niaba ya mgeni rasmi Samia Suluh Hassan amesema wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya wanao utajiri wa kutisha lakini athari zake kwa jamii ni kubwa, hivyo Watanzania lazima wachukue dawa hizo kwa nguvu zote.
"Kwa sasa uingizwaji wa dawa za kulevya nchini umepungua na ndio maana inaelezwa dawa kupanda bei kiasi cha wengine kuamua kuacha wenyewe na pale wanapopatikana wanaojihusisha na biashara hiyo wanakamatwa na sheria kuchukua mkondo wake wakati zamani wakikamatwa wanatoa rushwa na kuachwa,"amesema Mkuchika.
Hata hivyo amesema pamoja na mapambano ya dawa za kulevya kuwa na mafanikio makubwa Tanga inashika nafasi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya wanaojihusisha na dawa za kulevya na nafasi ya kwanza inashika na Dar es Salaam.Hivyo ameendelea kuishauri jamii ya Watanzania kushiriki kikamilifu kwenye mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Awali Kaimu Kamishna Jeneral wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Valite Mwachusa amesema kuwa mamlaka imeendelea kuweka mikakati ikiwemo ya kuhakikisha dawa za kulevya hazingizwi nchini , wakati mkakati mwingine ni kupunguza madhara yatonakayo na dawa za kulevya.
Mwachusa ameema pamoja na kufanikiwa kwa asilimia 90 kukabiliana na dawa za kulevya nchini bado tatizo ni kubwa na hivyo jamii ya Watanzania inayo nafasi ya kushiriki kikimalifu katika mapambano dhidi ya dawa hizo ambazo zikiachwa na kuingia nchini madhara yake ni makubwa.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...