KLABU ya  Azam FC, imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Kimataifa kutoka Burundi, Seleman Ndikumana, kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Nyota huyo amesaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', mmoja wa maofisa wa timu hiyo, Abubakar Mapwisa na wakala wa mchezaji huyo, Milner James.

Ndikumana aliyekuwa akichezea Al Adalah ya Saudi Arabia, ni mmoja wa washambuliaji wazoefu kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na ametua Azam FC baada ya kupendekezwa na Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije.

Hii ni timu ya pili kuwahi kucheza nchini Tanzania, nyingine ikiwa ni Simba aliyochezea 2006, pia akiwa na uzoefu barani Ulaya, akipita Molde ya Norway na FK Tirana ya Albania.

Huo ni usajili wa tatu kwa Azam FC, kwa ajili ya msimu ujao baada ya awali kulamilisha usajili wa wachezaji wengine wawili, winga Idd Seleman 'Nado' na kiungo mshambuliaji, Emmanuel Mvuyekure.

Kikosi cha Azam FC hivi sasa kipo kwenye maandalizi makali kujiandaa na michuano ya Kombe la Kagame, inayotarajia kuanza kutimua vumbi Julai 7 nchini Rwanda, ikiwa kama bingwa mtetezi wa michuano hiyo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat', akimkabidhi jezi mshambuliaji mpya wa Klabu hiyo Seleman Ndikumana baada ya kusaini kandarasi ya mwaka mmoja kutumikia klabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...