JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Description: Description: Description: Description: Description: Coat of Arms
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
Simu: 255-22-2114512, 2116898 
Baruapepe: press@ikulu.go.tz
Tovuti : www.ikulu.go.tz               

Nukushi: 255-22-2113425


OFISI YA RAIS,
      IKULU, 
 1 BARABARA YA BARACK OBAMA,   
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Ijumaa tarehe 28 Juni, 2019 amefanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Mhe. Verónica Nataniel Macamo Dlhovo, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro na Katibu wa Jukwaa la Wabunge la SADC Bi. Boemo Sekgoma.
Katika mazungumzo hayo, Mhe. Dlhovo ambaye ni Spika wa Bunge la Msumbiji amewasilisha salamu za Rais wa Msumbiji Mhe. Filipe Nyusi na salamu za Maspika wa SADC pamoja na kueleza kuhusu ushiriki wa jukwaa hilo katika Mkutano wa 39 wa SADC utakaofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Dlhovo amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi mzuri na hatua kubwa ambazo Tanzania inapiga katika maendeleo na ameeleza kuwa Jukwaa la Wabunge la SADC linakusudia kujenga mazingira ambayo yataweka sheria na taratibu zitakazowezesha nchi wanachama kubadilishana uzoefu ya kupiga hatua zaidi za maendeleo.
Aidha, Mhe. Dlhovo amesema Msumbiji na nchi nyingine za Afrika zinatambua mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania tangu wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika ukombozi wa mataifa mengi ya Afrika na uanzishaji wa nchi za mstari wa mbele na SADC.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Dlhovo kwa kufika Ikulu kumsalimu na kufikisha salamu za Mhe. Rais Nyusi na Wabunge wa SADC na amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zote wanachama wa SADC ikiwemo Msumbiji ambayo ina uhusiano wa kihistoria na kidugu na Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
28 Juni, 2019

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma ambao wameongozana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na wageni hao Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi zawadi ya picha ya Tingatinga na Kinyago Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, alipokutana na na kufanya mazungumzo naye Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya picha ya kuchora toka Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, huku akishuhudiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro alipokutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo, Katibu Mkuu wa Jukwaa hilo Mhe. Boemo Skgoma pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai na Naibu Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Ikulu jijini Dar es salaam  Ijumaa Juni 28, 2019
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipata picha ya kumbukumbu na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini kwa Afrika (SADC), Mhe. Veronica Nataniel Macamo Dlhovo pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mgeni huyo Ikulu jijini Dar es salaam Ijumaa  Juni 28, 2019 PICHA NA IKULU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...