Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya
wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Mongella
ametumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaodhani inauzwa kwa
gharama kubwa akisema nayo itashuka bei kama ilivyokuwa mifuko ya
"Rambo" ambayo wakati inaanza kutumika ilikuwa ikiuzwa kwa gharama kubwa
na baadae ikashuka.
Zoezi
hilo limefanyika katika eneo la Soko Kuu jijini Mwanza na kwenda
sambamba na uzinduzi rasmi wa matumizi ya mifuko mbadala ambapo wananchi
na wafanyabiashara wamehimizwa kuendelea kusalimisha mifuko ya plastiki
katika ofisi mbalimbali ikiwemo Serikali za Mitaa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye zoezi la kuhamasisha
katazo la Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko
(vibebeo) ya plastiki kuanzia leo Juni 01, 2019.
Mkuu
wa Wilaya Nyamagana, Dkt. Philis Nyimbi amewahimiza wananchi wa Wilaya
hiyo kuwa watiifu kutekeleza katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki na
kutumia mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Naibu
Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha amesema utekelezaji wa zoezi hilo
utazingatia sheria hivyo wananchi waondoe hofu kwani zoezi hilo
halitamuonea mtu yeyote na kwa wale ambao bado wana mifuko ya plastiki
waendelee kuipeleka katika ngazi husika kama ilivyoelekezwa.
Afisa
Mkaguzi kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC), Abel Sembeka akizungumza wakati wa zoezi hilo ambapo amesema
matumizi ya mifuko ya plastiki iliyozuiliwa ni ile inayohusisha vibebeo
kama vile "Rambo" na kwamba mifuko ya plastiki ya vifungashio kama
karanga, binzari na miwa bado haijazuiliwa.
Katibu
wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Nyamagana, akitoa salamu zake kwenye
zoezi hilo ambapo amesema Serikali itasimamia katazo la matumizi ya
mifuko ya plastiki kwa kuzingatia sheria hivyo wananchi wasiwe na
wasiwasi juu ya Serikali yao sikivu.
Viongozi
mbalimbali mkoani Mwanza wakifuatilia zoezi la kuhamasisha katazo la
Serikali kuhusu uzalishaji, usambazaji na matumizi ya mifuko (vibebeo)
ya plastiki.
Wananchi na wadau mbalimbali wa mazingira wakifuatilia zoezi hilo.
Wadau wakiwa kwenye zoezi hilo.
Viongozi wa dini, wafanyabiashara wadogo na wananchi wakifuatilia zoezi hilo.
Wananchi na viongozi mbalimbali wa dini wakinyoosha mikono kuunga mkono katazo la matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akionyesha mifuko mbadaya ambayo ni rafiki kwa mazingira inayopaswa kutumika.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya
viongozi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akimsikiliza mmoja wa akina mama wanaouza
mifuko mbadala jijini Mwanza ambapo Mongella amesema baada ya muda
mfupi ujao, mifuko hiyo itaanza kuuzwa kwa gharama nafuu baada ya
wafanyabiashara wakubwa kumaliza taratibu za kuitoa bandarini.
Mkuu
wa Mkoa Mwanza, John Mongella akigawa mifuko mbadala kwa baadhi ya
wananchi jijini Mwanza ili kuhamasisha matumizi ya mifuko hiyo.
Meneja
wa kiwanda cha Falcon kilichopo jijini Mwanza akionyesha baadhi ya
bidhaa ikiwemo mbao zinazotengenezwa kwa kutumia mifuko ya plastiki
ambapo amewahamasisha wananchi kukusanya mifuko hiyo na kwenda kuiuza
kiwandani hapo badala ya kuitapanya ovyo na kuharibu mazingira.
Baadhi
ya wajasiriamali wakisalimisha mifuko ya plastiki kwenye zoezi hilo
ambapo kampuni ya kufanya usafi ya GreenWestPro ilitumia zoezi hilo
kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kusalimisha mifuko ya plastiki.
Zoezi la kusalimisha mifuko ya plastiki likiendelea jijini Mwanza.
Wananchi
wameshauriwa kusalimisha mifuko ya plastiki katika ngazi husika ikiwemo
ofisi za Serikali za Mitaa badala ya kuitapanya ovyo na hivyo
kuhatarisha mazingira.
Kampuni
ya GreenWestPro ni mdau mkubwa wa mazingira ambapo inafanya shughuli
zake za usafi na utunzaji wa mazingira katika majiji matatu nchini
ambayo ni Dar es salaam, Mwanza na Dodoma.
Kampuni
ya GreenWastePro imetumia fursa hiyo kuhamasisha wananchi kuachana na
matumizi ya mifuko (vibebeo) ya plastiki na kujikita kwenye matumizi ya
mifuko mbadala ambayo ni rafiki kwa mazingira.
Tazama BMG Online TV hapa chini
Wananchi na wafanyabiashara watakiwa kusalimisha mifuko ya Plastiki
Ukikutwa na mifuko ya plastiki, adhabu yake ni hii hapa
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...