Wanafunzi zaidi ya 120 wa shule ya sekondari ya St Anne Marie Academy na Brilliant waliofaulu kwa daraja la kwanza na la pili kwenye mtihani wa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2018 wakiwa kwenye ukumbi wa zamani wa Bunge wa Msekwa wakipewa elimu kuhusu Bunge linavyoendeshwa. Shule hiyo imekuwa na utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi hao wanapofanya vizuri kwenye mitihani yao.

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

WANAFUNZI zaidi ya 120 wa Shule ya St.Anne Marie Academy na Brilliant ambao wamefanya vizuri katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, wametinga Bungeni, huku Spika wa Bunge Job Ndugai akiwapongeza kwa kufaulu kwenye masomo yao.

Akitangaza wageni waliotembelea Bunge Mjini Dodoma Spika Ndugai amesema wanafunzi hao wamefaulu kwa kupata daraja la kwanza na la pili kwenye matokeo hayo.

Amempongeza Mbunge wa Jimbo la Bukoba Vijiji(CCM), Jasson Rweikiza ambaye ndiye mmiliki wa shule hizo, kwa malezi mazuri kwa watoto hao ambao wameweza kufaulu kwa kiwango kikubwa na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Akizungumzia ziara hiyo ya kimasomo ya wanafunzi hao, Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura amesema kuwa wanafunzi hao wamepewa ziara hiyo kama motisha kutokana na kufanya vizuri sana kwenye mitihani yao.

Ameongeza wanafunzi waliopata fursa hiyo ni wanafunzi 29 wa St.Anne Marie waliopata daraja la kwanza na 59 waliopata daraja la pili na sita wa shule ya Briliant  waliopata daraja la kwanza na 20 waliopata daraja la pili.

Ndyetabura amesema imekuwa kawaida kwa shule hiyo kuwapa motisha wanafunzi wa shule hizo na ndiyo sababu shule imekuwa ikipata matokeo mazuri kwenye mitihani mbalimbali ya kitaifa.

Amesisitiza kuwa wanatarajia kuanza kuwapeleka nchini Dubai, Uingereza hadi Marekani wanafunzi watakaokuwa wanafanya vizuri kwenye mitihani yao ili iwe chachu kwa wengine kufanya vyema kwenye mitihani ya ndani na ile ya kitaifa.

"Shule imejiwekea utaratibu wa kuwapa motisha wanafunzi wanaofanya vizuri zaidi na huwa tunakawaida ya kuwapeleka mbuga za wanyama kama Serengeti, Mikumi, Ngorongoro hivyo tutaanza kuwapeleka Ulaya," amesema.
Mkurugenzi wa shule za Sekondari St. Anne Marie Academy na Brilliant ambaye ni Mbunge wa Bukoba Vijijini (CCM), Jasson Rweikiza kushoto Jasson Rweikiza akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo waliokwenda kutembelea bungeni Dodoma baada ya kupata daraja la kwanza na la pili kwenye matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018. Kulia ni Mbunge wa Sumve (CCM), Richard Ndasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...