Mhandisi Frederick Njavike ni Meneja wa wateja wakubwa Tanesco akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana namna ambavyo Shirika hilo limefanya ukaguzi wa mita zaidi ya 1000 katika maeneo mengi jijini Arusha ili kujiridhisha.
Zuberi Hassan ni Afisa Ukaguzi wa Mita amesema kuwa baada ya kufanya kama anavyoonekana akiendelea na ukaguzi huo ambapo wamegundua mita kadhaa zimechezewa ili zisiweze kusoma vizuri jambo ambalo ni hujuma kwa Shirika.
Na Vero Ignatus,Arusha.
Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mkoani Arusha limebaini kuwa zaidi ya Mita 1000 zimechakachuliwa mara baada shirika hilo kufanya Operesheni maalumu ya kukagua kubaini waliofanya hivyo ni njia ya kukwepa kulipa huduma stahiki za umeme hivyo wamechukuliwa hatua za kisheria
Zuberi Hassan ni Afisa Ukaguzi wa Mita amesema kuwa baada ya kufanya ukaguzi huo wamegundua kuwa mita kadhaa ambazo zimechezewa ili zisiweze kusoma vizuri matumizi ya umeme jambo ambalo ni hujuma kwa shirika hilo.
Joseph Shirima ni Mmiliki wa eneo ambalo lilikaguliwa na kukutwa na tatizo la mita kuchakachuliwa , amesema kuwa tatizo hilo lilisababishwa na baadhi ya wapangaji wasio waaminifu kufunga mita zao hivyo atashirikiana na shirika hilo ili kuhakikisha mita zinazowekwa zina kuwa na usahihi.
Mhandisi Frederick Njavike ni Meneja wa wateja wakubwa Tanesco amesema kuwa shirika hilo limefanya ukaguzi wa mita zaidi ya 1000 katika maeneo mengi jijini Arusha ili kujiridhisha na mita zilizopo pamoja na kuchukua hatua stahiki ikiwemo kusitisha huduma za umeme pamoja na kuchukua hatua Kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wateja wenye tabia ya kuchezea mita




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...