Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Kigoma

MAMLAKA ya Bandari Tanzania Kanda ya Ziwa Tanganyika, iko kwenye mchakato wa kurasimisha na kufunga bandari ambazo hazipo kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kigoma jana, Mkuu wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Ajuaye Msese alisema lengo la hatua hiyo ni kuzifanya bandari hizo zifanye kazi kulingana na kanuni na taratibu za kisheria na hivyo kuimarisha ulinzi na usalama.

"Utaratibu wa urasimishaji na kuzifunga bandari hizo bubu unaendelea na ukishamalizika tutazitangaza," alisema.

Pamoja na mambo mengine Msese alisema katika Bandari ya Kigoma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji lakini wamejipanga kukabiliana nazo kwa kuzitatua kimkakati.

Alizitaja changamoto hizo kuwa ni kupungua kwa shehena iendayo Nchi jirani za Congo na Burundi ambapo mkakati wa kutatua changamoto hiyo no kuendelea na juhudi za kutafuta masoko mapya na kuvutia yaliyopo.

"Changamoto nyingine ni ufanisi mdogo wa Shirika la Reli nchini (TRC), lakini mazungumzo ya pamoja kati ya Bandari ya Kigoma na TRC ili kuweza kuboresha miundombinu ya Reli kwa nia ya kuboresha huduma za usafirishaji," alisema Msese.

Akizungumzia huduma zinazotolewa na Bandari ya Kigoma, Msese alisema inatoa huduma kwa wateja aina mbili yaani wenye meli na wenye mizigo na nchi zinazohudumiwa na bandari hiyo ni Congo na Burundi.

Alisema bandari hiyo pia inahudumia shehena mchanganyiko, mafuta na makasha ambapo shehena hiyo imekuwa ikiongezeka licha ya matatizo ya njia ya usafirishaji hususani reli.

"Lakini pia katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi, mamlaka imeendelea kuboresha Bandari ya Kigoma kwa kufanya maboresho ya gati la abiria na upembuzi yakinifu ulishafanywa Kampuni ya M/S Royal Haskoning ya Uholanzi katika gati la mizigo umeshakamilika.

"Shirika la Misaada la Japan (JICA), litatekeleza mradi wa uboreshaji wa gati la abiria na ghala la kuhifadhia mizigo ambapo ujenzi huo utaanza Julai mwaka huu," alisema.
 Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwake Kigoma.
 Waandishi wa Habari  wakimsikiliza Meneja Bandari  Ziwa Tanganyika Ajuaye Msese.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...