Wote wanaotuma maombi ya kupata Visa kueleka nchini Marekani sasa watahitajika kutoa majina yao ya mitandao ya kijamii, anwani zao na nambari za simu katika sheria mpya zilizowekwa.
Kulingana na sheria mpya za idara ya maswala ya kigeni, wanaotuma maombi ya Visa watahitajika kutoa majina yao ya mitandaoni mbali na anwani za miaka mitano pamoja na nambari za simu.
Wakati sheria hiyo ilipopendekezwa mwaka jana, mamlaka ilikadiria kwamba itaathiri takriban watu milioni 14.7 kila mwaka.Hatahivyo baadhi ya wanadiplomasia na maafisa wanaotuma maombi ya kibali hicho huenda wakasamehewa.
Hatahivyo watu wanaoelekea Marekani kufanya kazi ama kusoma watalazimika kutoa habari zao .
''Tunajaribu kutafuta mikakati ya kuimarisha ukaguzi wetu ili kuwalinda raia wa Marekani , huku tukiunga mkono wale wanaosafiri kihalali'' , ilisema Idara hiyo.
Awali , ni watumaji maombi waliohitaji ukaguzi wa zaidi -kama vile watu waliosafiri katika maeneo yanayodhibitiwa na magaidi -ambao wangelzimika kutoa data hiyo.
Lakini asasa wanaotuma maombi watalazimika kutoa majina ya akaunti zao katika mitandao ya kijamii, mbali na kutoa maelezo ya akaunti zao katika mtandao yoyote.
''Mtu yeyote atakayedanganya kuhusu matumizi yao ya mitandao ya kijamii huenda akakabiliwa na adhabu kali ya uhamiaji'', kulingana na afisa aliyezungumza na The Hill.
Utawala wa rais Donbald Trump ulipendekeza sheria hizo mnamo mwezi Machi 2018.
Wakati huo, Muungano wa wanaraharakati nchini Marekani American Civil Liberty ulisema kuwa hakuna ushahidi kwamba ukaguzi huo wa mitandao ya kijamii unafanyika kwa njia ya haki na kusema kuwa hatua hiyo itawafanya watu kujizuia mitandaoni.
Trump aliahidi kuweka sheria kali za uhamiaji wakati wa kampeni ya uchaguzi wa 2016. Alitaka wahamiaji kufanyiwa ukaguzi wa kiwango cha juu wakati wa utawala wake.
KUSOMA ZAIDI BOFYA BBCSwahiili.com
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...