Na Ripota Wetu, Globu ya jamii.

 WAZIRI wa Waziri wa Fedha na Mipango wa Zanzibar Mohammed Ramia Abdiwawa ameishauri Kampuni ya Bima ya UAP kuendeleza utaratibu wake wa kuwa karibu na wateja wake ambao wanaopatikana Zanzibar.
Waziri Abdiwawa ametoa ushauri huo wakati wa futari ya pamoja iliyoandaliwa na kampuni hiyo ya bima ndani ya HotelVerde mjini hapo ambapo amesema wanaishukuru  kampuni hiyo kwa kuona umuhimu wa kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake kwa lengo la kuendelea kudumisha mshikamano uliopo baina yao.
 "Na ningeomba kwa hili niwapigie debe kwani ni Kampuni ambayo imekuwa na utamaduni huu kila mwaka na ninawaomba waendelee hivi hivi,"amesema Waziri Abdiwawa.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda ameelezea  umuhimu wa soko la Zanzibar kwa kampuni ya bima ya UAP na kusisitiza utaratibu huo wa kuwa karibu na wateja utaendelezwa kwani kwao wateja ni sehemu ya familia ya kampuni hiyo. "Hivyo basi wanastahili kukutana ili kudumisha familia yao hiyo kubwa inayozidi kukua siku hadi siku."
Wakati huo huo Mkuu wa kitengo cha fedha ambae pia ni Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nelson Rwihula ameishukuru Mamlaka ya bima Tanzania kwa kuendelea kuliendesha vizuri soko la bima hapa nchini.
Ghafla hiyo pia ilihudhuriwa na Naibu Kamishina wa Bima Tanzania Khadija Said ambaye amesema kwa utaratibu huo wa UAP na kuitaka pia iweze kushiriki katika masuala mengine pia ya kijamii pale inapowezekana
UAP ni kampuni ya bima yenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam. UAP ina matawi 9 yanayopatikana katika mikoa mbalimbali hapa nchini kama vile Dar Es Salaam, Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Kahama, Zanzibar, Morogoro na Mtwara.
 kiongozi wa tawi la Kampuni ya UAP Zanziba Farirah Saleh akisalimia wateja waliokuja kujumuika na kampuni hiyo. Kushoto kwake ni Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda baada ya kutoa hotuba ya kuwakaribisha wageni waalikwa pamoja na wateja wa kampuni hiyo ndani ya Hotel Verde Zanzibar.
 Mkuu wa kitengo cha Uendelezaji Biashara na Masoko Jabir Kigoda akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wateja baada ya kufuturu nao pamoja katika ghafla iliyoandaliwa katika Hotel Verde Zanzibar
 Naibu Kamishina wa Bima Khadija Said akiwasilisha hotuba yake katika hafla hiyo.
Menejimenti ya kampuni ya bima ya UAP ikiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya mawakala wa kampuni hiyo waliopo Zanzibar. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...