Na Zainab Nyamka, Michuzi Tv

UONGOZI wa Klabu ya Yanga Yanga kupitia Kamati za Utendaji na Hamasa kwa pamoja zimetangaza siku ya kuzinduliwa kwa jezi ya msimu wa 2019/20.

Hayo yamewekqa bayana leo na Katibu wa Hamasa wa Yanga Deo Mutta kutokana na wananchi kutaka kufahamu msimu ujao timu yao watavaa jezi gani.Mutta ameeleza kuwa aina ya jezi zitakazotumika msimu wa 2019/20 zitazinduliwa rasmi Wakati wa Wiki ya Mwananchi tarehe 01 Agosti mwaka huu.

Amesema kuwa, anatoa tahadhari kwa umma kwani mpaka sasa hakuna Jezi ya aina yoyote ambayo imeshatangazwa kwenye Chombo cha aina yoyote ile kwa hadi sasa hivyo wanayanga Wote Epukeni kabisa kununua Jezi au kifaa cha aina yoyote chenye Nembo ya Yanga kwakuwa muuzaji na mnunuaji wote niwahujumu wa mali za Yanga Kisheria.

Aidha, Mutta amesema Klabu tayari ilishamtangaza Msambazaji aliyekasimiwa dhamana hii kisheria kupitia Zabuni ambaye ni kampuni ya GSM.

Mutta amewataka wanachama na mashabiki wa Yanga kuepuka kushiriki kuihujumu nembo ya klabu yao kwa kununua bidhaa feki na kuikosesha Klabu mapato.
Katibu wa Hamasa wa Klabu ya Yanga Deo Mutta akielezea uzinduzi wa jezi za msimu wa 2019/20 utakaofanyika Agosti 01 mwaka huu na kuwatahadharisha wanachama kuacha kushiriki kuihujumu nembo ya Klabu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...