Na Woinde shizza Michuzi Tv, Arusha
Mbunge wa jimbo la Mikumi Joseph Mbilinyi (Prof Jay ) anatarajiwa kutumbuiza katika shindano la kumsaka mlibwende wa kanda ya Kaskazini linalotarajiwa kufanyika July 27 Karina ukumbi wa Naura Spring Jijini hapa.
Akizungumza na waandishi wa Habari Jijini hapa mkurugenzi wa kampuni ya kismat promotion media Ltd , ambaye pia ni Mkurugenzi wa mashindano haya Mary Mollel Alisema kuwa jumla ya warembo 12 waliotoka katika mikoa ya kanda ya Kaskazini ambayo ni Arusha, Tanga, Kilimanjaro na Manyara wanatarajiwa kuminyana katika usiku huo.
Alibainisha kuwa mbali na Profesa Jay kutoa burudani, Pia kutakuwa na wasanii mbalimbali kutoka Kanda ya Kaskazini zikiwemo ,burudani kutoka katika vikundi vya ngoma Za asili.
Ikiongea na warembo hao afisa Utamaduni jiji la Arusha Benson Maneno aliwataka warembo hao kujiandikisha Katika daftari la kudumu la kupiga kura kwani kwa kutokufanya hivyo watapoteza haki yao ya msingi ya kupiga Kura.
"pia napenda kuwasihi muwe na hekima na heshima na nithamu pia pindi mnapokuwa katika kambi zenu, muheshimu Jamii inayowazunguka pamoja na viongozi wanaowafundisha ,napia napenda kuwaasa muwe natabia Mjema maana nyie nimfano wa kuigwa katika Jamii naweza sema nikioo cha jamii "Alisema Maneno
Kwa wake mrembo wa kanda ya Kaskazini anaeachia muda wake Teddy Mkenda Alisema mashindano haya yamemsaidia mambo mengi ikiwemo kuvijua vituo mbalimbali vya utalii vilivyopo hapa nchini.
Hata hivyo aliwataka warembo hao kujiamini na kutumia taaluma yao na urembo huo kusaidia Jamii inayowazunguka, huku akiwataka kujitaidi ili waweze kuleta taji la miss Tanzania ndani kanda ya Kaskazini.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...