Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (kushoto)
akizungumza na wageni na wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom Tanzania Plc baada ya uzinduzi wa duka jipya la kampuni hiyo
lililopo Kigoma mjini hivi karibuni. Kampuni ya Vodacom ina maduka
takribani 100 na madawati ya huduma (Service desks) 350 na inaendelea
kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma
kirahisi zaidi. Kulia ni Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa Domician
Mkama, wengine ni watoa huduma wa duka hilo jipya.
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga (kushoto)
akisaidiwa kuweka alama ya kidole na Mkuu wa mauzo wa Vodacom Kanda ya
Ziwa, Domician Mkama kwa ajili ya kusajili laini ya mtandao huo wakati
wa hafla ya uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Kigoma mjini hivi
karibuni.
Mkuu
wa Mauzo wa Vodacom Kanda ya Ziwa, Domician Mkama (kushoto)
akizungungumza na wateja wa kampuni hiyo waliohudhuria uzinduzi wa duka
jipya la Vodacom lililopo kigoma mjini hivi karibuni. Kampuni ya
Vodacom ina maduka takribani 100 na madawati ya huduma 350 (Service
Desks) na inaendelea kupanua upatikanaji wa huduma ili kuwawezesha
wateja wake kupata huduma kirahisi zaidi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga na wengine pichani
ni watoa huduma wa duka hilo duka hilo jipya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...