Na Editha Edward-Tabora
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora imemuhukumu kujana mmoja kutumikia kifungo cha miaka Ishirini na miezi sita Jela anayefahamika kwa jina la Fabian Francis Mkazi wa Kaliua baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na nyara za Serikali ndani ya hifadhi ya msitu wa Ugalla wilayani Kaliua
Akisoma hukumu katika shauri hilo la uhujumu uchumi namba sita la mwaka 2019 hakimu mkazi Mfawidhi mkoa wa Tabora Chiganga Mashauri Tengwa amedai kuwa maamuzi hayo ya mahakama yamefikiwa baada ya kupitia maelezo ya pande zote mbili na kujiridhisha pasipo kuwa na shaka yoyote kuwa mshitakiwa Fabiani Francis amehusika kutenda makosa mawili baada ya kukutwa ndani ya hifadhi ya msitu wa Ugalla akiwa na nyara za Serikali nyama ya Wanyamapori
Katika Kosa la kwanza hakimu Chiganga Tengwa amemuhukumu kulipa faini ya Shilingi laki moja au Jela miezi sita huku Kosa la pili katika kesi hiyo Fabian amehukumiwa kifungo cha miaka Ishirini Jela
Awali katika mwenendo wa shauri hilo Wakili upande wa Jamhuri Tito Mwakalinga ameieleza mahakama kuwa mshitakiwa Fabiani Francis alikamatwa ndani ya hifadhi ya Ugalla Wilayani Kaliua eneo la upango mnamo tarehe 2 January 2019 akiwa na nyama ya wanyama wa porini yenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni nne na silaha ndogo kinyume cha sheria ya hifadhi ya wanyama pori.
Pichani ni kijana Fabian Francis aliyehukumiwa miaka Ishirini na miezi sita Jela kwa Kosa la kukutwa na nyara za serikali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...