Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv.
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili imewahikishia Wananchi kuendela kupata huduma za matibabu kwa gharama nafuu, huku ikieleza kuwa imeokoa shilingi bilioni 3.5 tangu kuwanza kutolewa kwa huduma ya upandikizaji wa figo Novemba mmwaka 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari, leo Agosti 2,2019 Daktari bingwa na mkuu wa idara kitengo cha figo Dkt.Jackline Shoo amesema toka walipoanza kutoa huduma hiyo yabkupandikiza fiho, ayari wagonjwa 47 wamepatiwa huduma hiyo ambayo imegarimu kiasi cha shilingi 1.1 bilioni.
Amesema, kama wagonjwa wote 47 wangepelekwa nje ya nchi basi kwa mgonjwa mmoja ingegharimu takribani shilingi milioni 80 hadi 100 na kufanya jumla yake kuwa shilingi bilioni 4.7 kwa wagonjwa wote. Lakini kwa huduma hiyo zaidi ya asilmia 25 hadi 32 ya fedha inaokolewa.
Aidha Dkt. Shoo amesema, wamekuwa wakipokea wagonjwa wengi wa figo lakini wengi wao hufika hospitalini hapo wakiwa wameshafikia hatua za mwisho kwani, kwa sasa tuna wagonjwa zaidi ya 300 ambao wanapatiwa huduma ya kusafishwa damu na karibu nusu yao wanahitaji huduma ya kupandikizwa figo.
"Hii ni mara ya kumi toka tulipoanza rasmi Novemba 2017 kutoa huduma hii, na kwa hatua ya leo wagonjwa wanne ambao wamepandikizwa figo akiwemo mtoto wa miaka tisa wanaruhusiwa kurudi nyumbani kuendelea na maisha yao ya kawaida Ila wanapaswa kuzingatia kutumia dawa kwani wagonjwa wote wanaopandikizwa na wale wanaotoa figo watatakiwa kuishi kwa masharti na kutumia dawa katika maisha yao yote", amesema Dkt Shoo.
Aidha Dkt Shoo alisema kuhusiana na garama za matibabu, wale wanaotumia bima zinalipia,lakini walioko kwenye msamaha wanapewa msamaha na ambao hawana uwezo kabisa hospital inagaramia
Kwa upande wake, Daktari bingwa wa figo Onesmo Kissanga amesema kila mwezi wamekuwa wakipokea wagonjwa takribani 20 wanaohitaji huduma maalum ikiwemo upandikizaji wa figo na kila wiki watoto 15 wamekuwa wakipokelewa wakiwemo watatu wanaotakiwa kupandikizwa figo au huduma maalum ya kusafishwa damu.
Alisema sababu ya kupokea idadi hiyo ya wagonjwa ni kutokana na changamoto ya elimu katika jamii kuhusiana na ugonjwa huo.Akizunguma kuhusu mtu anayepaswa kuchangia figo dkt Kissanga amesema anaetakiwa kufanya hivyo ni umchangia ndugu wa damu baada ya kufanyiwa vipimo na kuonekana kuwa vinafaa.
Naye, Mary Michael anayeishi Tanga ambae amemtolea figo mwanae Othniel Kimaro amesema ameamua kumtolea figo mwanae kufuatia hali yake ilikuwa siyo nzuri na kwamba alikuwa akipitia changamoto mbali mbali, lakini aliposhauriana na madaktari niliamua kumtolea mtoto wangu figo.
"Nililazwa hapa toka Alhamisi mtoto wangu akiwa na hali mbaya sana lakini baada ya kufanyiwa upandikizaji jumapili hivi sasa hana shida tena, mimi na mwanangu wote tunaendelea vizuri" ameongeza.
Mama huyo amewataka Watanzania kutoogopa kuchangia figo kwa ndugu zao wenye matatizo ya figo kwani kufanya hivyo wataokoa maisha ya ndugu zao kwani haina maadhara yoyote kwa kuwa huduma zinazotolewa hospitali hapo ni nzuri.Gasper Mbeka ambaye pia amepatiwa huduma hiyo, ameishauri serikali kuangalia namna ya kuweka utaratibu kwa ndugu wanofika kwa ajili ya kuwatolea ndugu zao figo kupatiwa husuma hiyo katika sehemu moja badala ya kuambiwa nenda Ocean road mara Agakhan kitendo kinachowafanya kushindwa kuwa wavumilivu na hats kifikia kuondoka.
Wagonjwa wengine waliofanyiwa upasuaji na kuruhusiwa leo ni pamoja na Ramadhani Ongoa.
Wataalam wa MNH wakiwa katika picha ya pamoja na wagonjwa waliopandikizwa figo na baadhi ya wachangiaji.
Wagonjwa waliopandikizwa figo wakiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Shoo kabla ya kurejea nyumbani leo.
Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Jacqueline Shoo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu huduma ya upandikizaji figo ambayo ilianza Novemba, 2017.
Mkazi wa Tanga, Merry Michael akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu afya ya mtoto wake, Othniel Kimaro baada kupandikizwa figo Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mtoto huyo amechangiwa figo na mama yake, Bi. Merry Michael.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...