Na Evelina Odemba, Ofisi ya DED Sikonge

WATU wawili raia wa Afrika Kusini wamefariki katika ajali ya ndege iliyotokea mapema asubuhi ya leo majira ya saa moja na nusu katika kata ya Igigwa Wilayani Sikonge mkoani Tabora.

Watu hao waliotambulika kwa majina ya D. Werner mwenye umri wa miaka 58 pamoja na Werner Fredrick Fronaman mwenye umri wa miaka 36 wote wanaume na raia wa Durban Afrika ya kusini walikuwa kwenye ndege yenye namba za usajili 19-ZU-TAF mali ya Afrika Kusini.

Akielezea tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Sikonge Mhe. Peres Magiri alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo na kusema kuwa ambao walikuwa katika ziara ya kuhamasisha wanafunzi barani Afrika kusomea maswala ya Anga.

Kabla ya ajali kutokea hapo jana walitua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Tabora wakitokea Entebe Uganda kuelekea Lilongwe Malawi ili kufika Afrika ya kusini. 
Asubuhi ya leo walipoanza safari baada ya muda mchache walifanya mawasiliano na wataalamu wa uwanja wa ndege wa Tabora na kutoa taarifa kuwa injini ya ndege imezimika ghafla wakiwa angani hivyo wanafanya utaratibu wa kurudi Tabora.
Baada ya taarifa hizo hawakuweza kupatikana mpaka  taarifa ya ajali hiyo ilipopokelewa na walipofika ene la ajali wakakuta watu  hao wameshafariki.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...