KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imempongeza Rais Dk. John Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), na lugha ya Kiswahili kukubalika kuwa lugha ya nne kwenye jumuiya hiyo.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Tanzania, Dominic Dhanah wakati wa hafla ya kufunga mkutano wa 39 wa SADC ulioshirikisha nchi 16 za jumuiya hiyo.Mkutano huo umefungwa leo na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Dk.Magufuli.

Akizungumza baada ya kufungwa kwa mkutano huo, Dominic Dhanah amesema Tanzania ni moja ya nchi ambayo wanafanya vizuri katika soko la mafuta na vimiminika, hivyo kitendo cha Rais Magufuli kuwa mwenyekiti kitawaongezea nguvu ya kufanya kazi kwa upana mkubwa.

“Puma Energy Tanzania tunampongeza Rais Magufuli kuwa Mwenyekiti wa SADC, lakini pia hili la Kiswahili kuwa lugha rasmi ya jumuiya hii ni la kupongezwa na kuungwa mkono kwani ni wazi Kiswahili kitasambaa kwa kasi,” alisema Dhanah.

Amesema Kampuni ya Puma inafanya kazi kwenye nchi 13 wanachama wa SADC hivyo ni imani yao kuwa juhudi anazozionesha Rais Magufuli kujenga uchumi na maendeleo ya nchi zitasambaa kwa nchi nyingine.

Ameongeza mikakati yao ni kuhakikisha kuwa wanafikia nchi nyingine zilizobaki ili kushika koso zima la kanda hiyo ya jumuiya ya SADC.

Mkurugenzi huyo amesema katika kuonesha mchango wao kwa SADC walitoa shilingi milioni 300 kwa ajili ya kugharamia mkutano huo wa 39.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya mafuta ya Puma Energy Tanzania akizungumza na vyombo ya habari wakati akitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).Pongezi hizo amezito baada ya Rais Dkt Magufuli kufunga mkutano wa Jumuiya hiyo Agosti 18,2019 uliofanyika katika kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere,jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...