Rais wa Zambia Mh. Edgar Changwa Lungu, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) pichani kati akiongoza kikao cha ulinzi na usalama kwa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika – SADC (SADC) kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika – SADC, Dkt Stergomena Tax.
Rais wa Angola Mh. Joao Lourenco Mwenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) anayemaliza muda wake akiwa katika kikao hicho kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Rais wa Zimbabwe Mh. Emmerson Dambudzo Mnangagwa anayechukua nafasi ya Uenyekiti wa Taasisi ya Siasa, Ulinzi na Usalama (SADC Troika) akipitia baadhi ya nyaraka za kikao hicho kilichofanyika jioni ya leo kwenye ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...