Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde 

Na Charles James, Michuzi TV.

Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira imekuja na mkakati wa kuwawezesha Vijana kushiriki katika uchumi wa Viwanda kwa kusambaza malighafi za viwandani zitokanazo na kilimo kwa lengo la kutatua changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa kundi la Vijana.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde katika Kijiji cha Duluti-Wilaya ya Kibaha wakati akikagua Shamba la Ekari 50 ambalo litatumiwa na Vijana kulima maembe ambayo yatanunuliwa na Kiwanda cha Sayona Drinks kilichopo Kijiji cha Mboga,Wilaya ya Bagamoyo.

"Tumeongea na Kiwanda cha Sayona ambao wameonesha utayari wa kuwawezesha vijana hawa mbegu za maembe na kuwachimbia kisima kuwa soko kuu la maembe yatakayozalishwa shambani hapo.

Huu ni mkakati ambao tumeuweka kwa kuishirikisha sekta binafsi kwenye kutatua changamoto za Ukosefu wa Ajira miongoni wa Vijana na hivyo tumeshatembelea viwanda vingi hapa nchini na vimeonesha nia ya kushirikiana na serikali katika mpango huu" amesema Mavunde.

Akitoa maelezo kwa niaba ya Wananchi,Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Mh Humud Jumaa ameishukuru Serikali kwa mpango wake huo madhubuti wa kutatua changamoto za ajira kwa vijana na kuahidi kuwasaidia Vijana hao kuwa katika mfumo rasmi wa vikundi ili wawezeshwe kupitia mifuko mbalimbali ya serikali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...