
Na.Khadija seif, Michuzi tv
MSANII wa kike wa Bongofleva pamoja na Bongomovie kwa pamoja Zuwena Mohammed a.k.a shilole amikiri wazi kushuka kwa soko la Muziki kwa kipindi hiki.
Akizungumza kwenye vyombo vya habari hivi karibuni ,Shilole amesema kwa sasa anakumbana na changamoto ya kutotoa ngoma mpya kutokana na kutokuwepo kwa mpangilio mzuri sokoni kwani kila Msanii anatoa ngoma mpya kiasi kwamba inapelekea mashabiki kutoweza kutegea sikio nyimbo ipi na kupata wasaa wakuburudika.
"Imekua changamoto mpaka kwa watayarishaji (producer) kuchanganya vionjo na kuvirudia rudia kwa nyimbo zaidi ya moja,"
Hata hivyo shilole amewatolea uvivu waandaaji wa tamasha la wasafi kutokana na kubagua baadhi ya wasanii kutokuwepo kwenye tamasha hilo tangu lianze kwa mwaka huu.
"Wajaribu kuwa sawa na kufata utaratibu kama waandaaji wa Matamasha mengine walivokua wakifanya hasa katika kuchagua wasanii watakaotumbuiza kwenye jukwaa lao pindi wanaposafiri mikoani kwani kwa sasa soko la Muziki limekua pana sana na wasanii chipukizi ni wengi na wanafanya vizuri sana,"
Aidha amesema kundi la lebo ya wasafi wamekua wakijipendelea wao wenyewe kutokana na uwezo waliokua nao hivyo amewashauri kusaidia na wasanii wengine kujiinua kimuziki na kutambulika ndani na nje ya nchi Kama wasanii waliomo kwenye kundi hilo Rayvan,lavalava, Harmonize pamoja na Mbosso ambae amekua akipewa ushirikiano mkubwa kutoka kwenye lebo hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...