Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv
SERIKALI imesema kupitia mkutano wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika(SADC).
Itahakikisha inatumia kamati mbalimbali za SADC kuwasaidia wabunifu katika Sayansi na teknolojia ili waweze kufanya tafiti zenye kuleta tija na kutatua changamoto za jamii nchini
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameyasema hayo leo Agosti Mosi, jijini Dar es Salaam, katika kilele cha maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Amesema, zipo kamati mbali mbali za mawaziri wa sayansi na teknolojia pamoja na ubunifu ambapo wamepanga mipango ya kuendeleza ubunifu na kwamba wanaangalia na kuweza kuwatambua wabunifu kwa kuwaendeleza.
Ameongeza kuwa serikali imeweka mipango na taratibu madhubuti za kuwatambua wanasayansi na wabunifu hasa kipindi hiki ambacho jumuiya hii inaingia katika Mapinduzi ya Viwanda na kufanya wabunifu kuwa ni watu wa muhimu na kuongeza kuwa, maonesho hayo ya TYS, yanaashiria kuwa elimu inayotolewa inakidhi na kuwa na uwezo wa kutatua changamoto za jamii hasa katika masomo ya Sayansi.
"Nimefurahi kuona miradi inayoonyeshwa imeongezeka kutoka 81 na hadi 95 ambayo ni mafanikio makubwa kwa sekta hii..."Najivunia kuona kuwa idadi ya wasichana imezidi kuongezeka kwani mwaka huu wasichana 88 waliojitokeza kushiriki maonesho haya ni sawa na asilimia 46," amesema Ndalichako.
Pia amewapongeza wasichana wanaozidi kujitokeza katika mambo ya sayansi Teknolojia na ubunifu kwani zamani masomo ya Sayansi hayakupendwa na wasichana lakini katika kipindi hiki mwamko umekuwa mkubwa kutokana na jitihada za walimu kuhamasisha Sayansi mashuleni.
Profesa Ndalichako pia amewaomba walimu kuwafundisha wanafunzi kufanya tafiti ambazo zitasaidia ukuaji wa uchumi hasa katika Mapinduzi manne ya Viwanda kwani hata tafiti zilizofanyika kwa mwaka huu zimekuwa na kiwango bora na zenye kulenga kutatua changamoto zilizopo katika jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Dk. Amos Nundu amesema kwa muda mfupi vijana kupitia YST wamefanya tafiti zinazoonesha kutatua changamoto za jamii.
"Mifumo huu ni mzuri kwa kuwa umeweza kujenga vijana wadogo wenye uwezo wa kufanya tafiti zenye weledi zinazosaidia kuchangia ukuaji wa taifa," alisema Dk. Nundu.
Naye, Mkurugenzi Mkazi wa mfuko wa kusaidia ubunifu Tanzania (HDIF) Joseph Manirakiza amesema, wao kama wadau wa ubunifu nchini,
wamekiwa wakiiunga mkono YST kwa miaka 4 sasa. "Sisi HDIF tunafanya hivi kwa sababu tunaamini katika mchango wa ubunifu kwa maendeleo ya nchi yoyote, na ukianza kuwajenga vijana wakiwa wadogo una uwezekano mkubwa wa kuja kuwa na wanasayansi, wagunduzi na wabunifu wengi wazuri mbeleni", amesema Manirakiza
Katika maonesho hayo Washindi walikabidhiwa vikombe na medali ambapo mshindi wa Kwanza ilikuwa ni shule ya Sekondari ya Chief dodo ya mkoani Manyara ikifuatiwa na shule ya Sekondari Kisimiri na Iliboru.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wandau mbalimbali wa elimu leo Agosti Mosi katika kilele cha maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mkurugenzi Mkazi wa mfuko wa kusaidia ubunifu Tanzania (HDIF) Joseph Manirakiza akikabidhi zawadi kwa washindi wa tuzo ya human development innovation katika kilele cha maonesho ya Young Scientists Tanzania,leo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu na Mafunzo yab Ufundi,Prof Joyce Ndalichako akipata maelezo mafupi kutoka kwa wanafunzi walioshili maonesho ya tisa ya wanasayansi chipukizi Tanzania (YST) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.(Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi Tv)
Mtaalamu wa mambo ya Mahusiano kutoka HDIF, Hannah Mwandoloma akifafanua jambo kwa wanafunzi katika maonesho hayo.
Mtafiti Msaidizi wa Ubongo Kids, Timothy Sambwe, akifafanua jambo kwa wanafunzi waliotembelea banda la HDIF kujua jinsi katuni za mbali mbali za masomo maarufu kama ubongo kids zinavyobuniwa. Ni katika maonesho ya wabunifu chipukizi yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam
Mtaalamu wa mambo ya Mahusiano kutoka HDIF, Hannah Mwandoloma akifafanua jambo kwa wanafunzi katika maonesho hayo.
Mtafiti Msaidizi wa Ubongo Kids, Timothy Sambwe, akifafanua jambo kwa wanafunzi waliotembelea banda la HDIF kujua jinsi katuni za mbali mbali za masomo maarufu kama ubongo kids zinavyobuniwa. Ni katika maonesho ya wabunifu chipukizi yaliyomalizika leo jijini Dar es Salaam
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...