Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia) akifafanua jambo kwa mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya wakati Mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe na kujadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana ili kuinua soka la Tanzania.

Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (kushoto) akimwelezea Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe mikakati ya Shirikisho la nchi yake katika kuisadia Tanzania kufanya vizuri katika mchezo wa soka.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi nchini, Boniface Wambura (kushoto) akifafanua kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) mikakati mbalimbali waliyofikia na Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (hayupo pichani) wakati mjumbe huyo alipomtembelea Waziri Mwakyembe leo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (kulia)akiagana na Mjumbe kutoka La Liga nchini Hispania, Alvaro Paya (kushoto) mara baada ya kumaliza kujadiliana mambo mbalimbali ya kushirikiana ili kuinua soka laTanzania.Picha na WHUSM-Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...