Na Ripota Wetu-Mkoa wa Katavi.
Kufuatia harambee iliyoandaliwa kuanzi tarehe 26/8/2019 hadi kilele chake tarehe 6/9/2019 katika chakula cha hisani kuchangia ukarabati wa Hospitali teule ya rufaa ya Katavi.
Tarehe 6/9/2019 Homera Marathon imehitimishwa kwa kupatikana jumla ya Tsh. Milioni Miambili, Arobaini na Mbili na Sitini na Nne Elfu,Miatano na Sabini (Tsh 242,064,570) na kuvuka lengo lililohitajika la million 194).
Akitangaza kiasi hicho katika ukumbi wa Police Club wakati wa chakula cha hisani Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Juma Zuberi Homera amesema hiyo ni jumla kuu ambapo kiasi hicho ni fedha taslimu na ahadi.
RC Homera amesema, kiasi hicho kimevuka malengo ambapo amesema ili ukarabati ukamilike ilikuwa inahitajika Tsh. Milioni Mia Moja,Tisini na Nne Elfu (Milion194) na amewaomba walioahidi wakamilishe ahadi zao ndani ya Wiki moja ili ukarabati uanze haraka iwezekanavyo.
Aidha, amewashukuru Wananchi wa Mkoa wa Katavi, wafanyabiashara, Wabunge na viongozi wote kwa ujumla lakini pia amewashukuru na Wafanyabiashara wa katavi na nje ya katavi, Watumishi wa umma na Taasisi za serikali na zisizo za kiserikali, Bank za NMB,TPB, CRDB, NBC, Waandishi wa Habari, na pia amevishukuru Vyombo vya habari yakuitangaza Homera Marathon na dhamira ya Mkoa huo kufikia kilele chake tarehe 6/9/2019.
Ikumbukwe pia kabla ya chakula cha hisani, Asubuhi kulikuwa na mbio za KM 1,3,5,10 na KM 20 ambapo washindi watatu wa KM 5 wa kwanza alipewa Tsh 50,000/= mshindi wa Pili Tsh 30,000/= na watatu Tsh 20,000/= sanjari na kutunukiwa vyeti na medani.
Waliokimbia KM 10 mshindi wa Kwanza Tsh 70,000/=, Mshindi wa Pili Tsh 50,000/= na mshindi wa Tatu Tsh 20,000/=.
Waliokimbia KM 20 mshindi wa kwanza na wa pili walifanafana ambao kila mmoja amepewa Tsh 100,000/=, Mshindi wa Pili Tsh 70,000/= na mshindi wa Tatu Tsh 50,000/= zawadi zilizokabidhiwa na Mkuu wa Mkoa.
Mwisho Burudani ziliendelea kutoka kwa waimbaji wa Kimataifa wa nyimbo za Injili Christopher Mwahangila, Sifael Mwabuke, Ambwene Mwasongwe pamoja na Zabron Singers kutoka Shinyanga.




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...