Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni,Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam wakati alipoelezea kusikitiswa kwake na suala zima la kutopewa nafasi kuutumia uwanja wa Taifa kwa ajili ya Tamasha la Pasaka.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Bw Alex Msama Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni wakati akizungumza nao leo ofisini kwake Kinondoni jijini Dar es salaam.
......................................................
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni ya jijini Dar es salaam inayoandaa matamasha ya muziki wa injili Tamasha la Pasaka na Tamasha la Krismass Bw. Alex Msama amesema anasitisha kwa muda uandaaji wa matamasha hayo katika jiji la Dar es salaam.
Msama amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kunyimwa kibali cha kuutumia uwanja wa Taifa unaomilikiwa na Serikali kwa muda wa miaka mitatu sasa.
"Tangu mwaka 2017-2019 nimekuwa nikiandika barua kwenda wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuomba kuutmia uwanja huo bila mafanikio,na barua zote ambazo tumekuwa tukiwaandikia hazikuwahi kujibiwa mpaka sasa",alisema Msama
Amesema kuwa Tamasha la Pasaka linachukua zaidi wa watazamaji 45,000 watu ambao ni wengi sana, hivyo maeneo mengine hayawezi kutosheleza zaidi ya uwanja wa Taifa au uwanja wa Uhuru.
Akifafanua kwa ufupi kwa njia simu Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema Wizara hiyo ni pana na ina mambo mengi, Hivyo yeye hana taarifa zozote kuhusiana changamoto hiyo.
Mwakyembe amesema muhusika anaepokea barua zote za Wizara ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo hivyo akawataka Wanahabari kuwasiliana na Katibu Mkuu kupata ufafanuzi zaidi wa jambo hilo.
Michuzi Blog inaendelea na juhudi za kumtafuta Katibu Mkuu kutoa ufafanuzi kuhusu changamoto hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...