Na Ripota Wetu, Michuzi TV

ASASI mbili za kiraia za Action for Change(ACHA) na The Right Way (TRW) zinatarajia kupeleka waangalizi jumla ya 215 katika Wilaya zote za Tanzania Bara kwa ajili ya kufuatilia mwenendo wa uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajia kufanyika Novemba mwaka huu.

Pia imeelezwa ACHA na TRW kwa pamoja wanadhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia na uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2019 sanjari na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ili kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru zaidi, za haki za kuaminika Tanzania.

Akizugumza leo jijini Dar es Salaam kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 na Uchaguzi Mkuu wa 2020,Ofisa Mradi wa ACHA Jackson Sikahanga amesema wanatarajia kupeleka waangalizi hao kuhakikisha wanafuatilia mchakato mzima wa uchaguzi wa Serikali za mitaa.

"ACHA TRW tuna matarajio kwamba uchaguzi huu utakuwa huru, haki , kuaminika , tulivu na wenye amani.Pia utakuwa wa uwazi na utakaoshirikisha makundi maalumu , mfano watu wenye ulemavu, wanawake, vijana na wazee.

"Ni dhahiri kuwa uangalizi wa uchaguzi huu utafanyika pia kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa na mafunzo bora yatakayotolewa kwa wakati katika nyanja zote za michakato ya uchaguzi na hata baada ya uchaguzi,"amesema na kuongeza uangalizi na umakini huo katika utoaji taarifa vitabainisha maeneo yenye ucdhaifu kwa marekebisho kwa siku zijazo

Sikahanga amesema ACHA na TRW zinalenga kuona mchakato wa uchaguzi unaofuata viwango vya kitaifa na kimataifa, kama ambavyo Tanzania imeridhia na zile zilizopo kwenye sheria za manispaa , kanuni na miongozo kutoka vyombo mbalimbali vya kusimamia uchaguzi ikiwemo Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC).

Pia amesema uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na uchaguzi mkuu mwaka 2020 ni fursa nyingine kwa Watanzania kushuhudia ukuaji wa utawala wa demokrasia. Aidha amesema ipo haja ya ushiriki mpana wa wananchi wote katika mchakato wa uchaguzi, kaunzia kipindi kabla ya uchaguzi kwa mfano uandikisha waji wa wapiga kura, elimu ya mpira kura na uteuzi katka vyama.

"Mchakato huu unahitaji mfumo wa mwenendo thabiti wa elimu kwa wananchi katika zoezi zima, ambalo litafanya elimu kwa mpiga kura kuwa thabiti na wenye tija , mwamko huu wa wananchi kupitia elimu kwa umma na programu ya mpiga kura , ambayo imeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuwadaidia wananchi kutambua kuwa ushiriki katika uchaguzi ni haki yao,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRW Rhoda Kamungu amesema upo ushahidi usiojitosheleza unaunga mkono umuhimu wa vyombo katika kuhakikisha Serikali inawajibika juu ya utawala bora ,haki na misingi yote ya haki za binadamu na kwa wananchi wake.

"Ni jukumu letu kuwajulisha wananchi kama nguzo muhimu kupitia vyombo vya habari katika kutoa jukwaa jumuishi la mjadala wa umma na majadiliano kuhusu kuhamasisha mijadala kwa kuzingatia Katiba,sheria,sera ,taratibu na miongozo.Utafiti unadhihirisha kuwepo idadi kubwa ya wapiga kura wasiofahamu kuhusu mchakato na utaratibu wa uchaguzi,"amesema.

Kuhusu kwanini elimu ya uraia, elimu ya mpiga kura na ungalizi ni muhimu, Kamungu amejibu kuwa ACHA na TRW kwa pamoja wanatamani kuona mchakato wa uchaguzi ambao unaongozwa na wananchi, shirikishi , wenye uwazi , huru na haki. "ACHA na TRW tutatoa elimu ya uraia, mpiga kura na uangalizi wa michakato ya uchaguzi kwa kuzingatia vigezo vilivyopo.
 Mkurugenzi wa The Right Away ,Rhoda Kamungu  akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam,mambo mbalimbali ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi mkuu,sambamba na namna  Asasi hizo zilivyojipanga kupeleka waangalizi  Wilaya zote za Tanzania Bara,ambapo ameeleza kuwa waangalizi wa Muda mrefu  wapatao 215 watapewa jukumu hilo ngazi ya majimbo na Waangalizi wa muda mfupi wapatao 3600 watapelekwa kwenye vituo mbalimbali vya uangalizi nchi nzima.
 Ofisa Mradi wa Action for Change   (ACHA) Jackson Sikahanga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  namna walivyodhamiria kuendesha mpango wa pamoja wa kutoa elimu ya uraia,na uangalizi wa uchaguzi wa Serikali za mitaa kwa mwaka 2019 sanjari na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ili kuzifanya chaguzi hizo kuwa huru zaidi, za haki na kuaminika Tanzania.



 Ofisa Mipango wa ACHA na TRW akitolea ufafanuzi wa baadhi ya mambo yalitozungumza na Watangulizi wake kwenye mkutano huo na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...