Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii
WAKATI upelelezi wa kesi ya mauaji inayomkabili mfanyabiashara Hamis Said (38) anayedaiwa kumchoma mke wake na magunia mawili ya mkaa umekamilika, wakili Mohamed Majaliwa amejitambulisha mahakamani hapo kama wakili wa utetezi wa mshtakiwa .
Mapema wakili wa serikali Mwandamizi, Wankyo Simon aliiarifu mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini upelelezi umekamilika na kwamba jalada la kesi hiyo liko kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya kuletwa ofisi ya taifa ya mashtaka kusoma.
Simon alidai kuwa jarada la shauri hilo lipo kwenye hatua ya uchapaji kwa ajili ya maandalizi ili lipelekwe Mahakama Kuu ya Tanzania hivyo aliiomba mahakama hiyo ihairishe kesi hiyo.
Kufuatia taarifa hiyo, hakimu Mkazi Mkuu, Salum Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 4,2019
katika kesi ya msingi mshtakiwa anakabiliwa na kosa moja la mauaji ambapo anadaiwa Mei 15, 2019 katika oneo la Geza Ulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...