Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekamata silaha mbili aina ya Short Gun zikiwa na risasi mbili ambazo zilikuwa kwenye mtutu wa kila silaha ambazo zilikuwa zimefichwa kwenye mfuko wa plastiki.

Kufuatia msako mkali uliofanyika Oktoba 17, 2019 saa 17:00 jioni huko maeneo ya Pambogo, mtaa wa Isengo, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya, Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilikamata silaha hizo ambazo zimetengenezwa kienyeji na baada ya kuzikagua zilibainika kutokuwa na namba za usajili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ninatoa rai kwa wananchi kutoa taarifa za mtu/watu au kikundi cha watu ambacho wanakitilia mashaka katika maeneo yao ili ufuatiliaji ufanyike. Aidha ninatoa rai kwa mtu yeyote anayemiliki silaha kinyume cha sheria kusalimisha silaha hiyo mara moja kituo cha Polisi kwani Jeshi la Polisi tunafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha usalama wa raia na mali zao ndani ya Mkoa huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...