MAHAKAMA
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewaamuru washitakiwa tisa wanaokabiliwa na
kesi ya wizi wa katoni 700 za korosho kulipa fidia ya Sh.milioni 125
kama hasara waliyoisababisha kwa Serikali.
Washitakiwa
hao ni Robert Slaa, Isihaka Ngubi, Cathbert Mlugu, Mrisho Mindu,
Mauridi Haji, Hamza Bunda, Kelvin Ngwandu, Joseph Robert na Joseph
Mihayo wamesomewa adhabu hiyo leo Oktoba 23,mwaka 2019 baada ya kuomba
msamaha na kukiri makosa yao.
Akisoma
adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi amesema washitakiwa wote
wataachiwa huru kwa sharti la kutofanya kosa lolote kwa muda wa mwaka
mmoja pia amewataka watimize masharti ya makubaliano yanayowataka
kulipa hasara ya korosho walizoiba.
Katika
kesi hiyo, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa kati ya Januari 26 hadi
Februari 6, 2018 katika yadi ya Kampuni ya Zambia Cargo and Logistics
Limited, waliiba katoni 700 za Korosho zilizobanguliwa zenye thamani ya
Dola za Marekani 54,180 sawa na zaidi ya Sh.milioni 125.
Ilielezwa kuwa korosho hizo zilikuwa mali ya Barabara Trading Tanzania Limited na zilikuwa zikisafirishwa kwenda nchini Vietnam.
Ilidaiwa
washitakiwa waliiba katoni hizo za korosho zilizokuwa katika kontena na
kisha kuyajaza mchanga na mengine kuyaacha matupu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...