Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Tandahimba Ahmada Suleiman amewataka watendaji wa kata na vijiji kufuata mwongozo wa kanuni za uchaguzi katika kugawa fomu za wagombea katika maeneo yao
Hayo ameyasema kwenye semina ya watendaji wa kata na vijiji iliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Tandahimba
"Tumieni kanuni za Uchaguzi katika kugawa fomu kwa wagombea haki itendeke kwa kila mgombea na baadhi ya watendaji msifanye kazi kwa mazoea kwakuwa kila Uchaguzi una mambo mapya,"alisema Suleiman
Alisema wagombea wajitokeze kuchukua fomu kuanzia kesho tarehe 29 Oktoba katika maeneo yao ya kata na vijiji.
Watendaji wakihakiki fomu za wagombea ambazo wanakwenda kugawa kwenye maeneo yao
Muwezeshaji Zuberi Sarahani akiwasisitiza Watendaji kutumia kanuni za uchaguzi
Watendaji wa kata na vijiji wakimsikiliza muwezeshaji.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...